Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. John Mnyika akiwa amebebwa juu juu na Wanachana wa Chama hicho pamoja na washabiki wake nje ya Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam leo mara baada ya kushinda kesi yake iliyokuwa ikimkabili kuhusiana na Ushindi wake kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Mnyika akipongezwa na Baadhi ya jamaa zake waliofika Mahakamani hapo.
Wanachama wa Chadema pamoja na washabiki wa Mbunge wa Jimbo la Ubungo wakishangilia ushindi wa kesi ya Mbunge wao,Mh. John Mnyika.
Askari Polisi wakihakikisha usalama upo wa kutosha katika njia walizokuwa wakipita wapenzi wa Chadema kusherehekea ushindi wa Mbunge wao.
Mh. Mnyika alipokuwa akiwasili Mahakamani leo asubuhi.
Post your Comment