
Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela akiwa anaapa kiapo cha utiifu mbele ya mkuu wa mkoa wa arusha Magesa Mulongo leo

Akuu wa wilaya ya Arumeru Nyirembe Munasa akiwa anakula kiapo cha uaminifu mbele ya mgeni rasmi


Wakuu wa wilaya wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Arusha
Katika jiji la Arusha leo wakuu wapya wilaya wameapishwa ambapo Mkuu wa mkoa wa Arusha magesa mulongo amewaotaka wasiliwe sifa na badala yake wahakikishe kuwa wanajikita zaidi katika kutatua kero za wananchi.
Mbali na hayo aliwataka washirikiane na Madiwani katika kutatua tatizo la hati chafu ndani ya halmashauri kwa kuwa kati ya halmashauri zote jijini hapa iliyo na hati safi kidogo ni halmashauri ya Meru pekee
Pia aliwataka wakuu hao kuhakikisha hawapigwi chenga na sheria mbalimbali hasa za vijiji na ile ya asilimia ishirini kwa kila lkijiji kwa kuwa kwa sasa halmashauri zinakwepa sheria hiyo na hali hiyo inapelekea wenyeviti wa vijijiji kuwa katika hali nghumu ya kiutendaji
Post your Comment


