Get the latest updates from us for free

mas template
Home » , , , » Obama amwalika Kikwete kushiriki mkutano wa G8

Obama amwalika Kikwete kushiriki mkutano wa G8

Written By mpekuaji on Wednesday, May 16, 2012 | 9:51:00 AM


Mwandishi Wetu, Washington DC
RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwasili leo mjini hapa kwa ziara ya kikazi ya siku tano kwa mwaliko wa Rais Barack Obama wa Marekani, ambayo pamoja na mambo mengine, atashiriki mkutano wa Nchi Nane Tajiri Duniani (G8) utakaofanyika Camp David na kuhutubia mkutano wa dunia kuhusu usalama wa chakula. 

Rais Kikwete ni miongoni mwa marais wanne wa Afrika walioalikwa kwa ajili ya mkutano huo. 


Wengine ni Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Yayi Boni wa Benin, Rais John Mills wa Ghana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi. Viongozi hao wa Afrika wanatarajiwa kusaini hati ya makubaliano ya awali na viongozi wa G8 mwishoni mwa mkutano wao. 

Kongamano hilo la kila mwaka la “Kilimo Duniani na Usalama wa Chakula” litafunguliwa na Rais Obama, na Rais Kikwete na viongozi wengine wanatarajiwa kujadili hatua za kuimarisha uzalishaji chakula katika Afrika. 

Aidha, Rais Kikwete anatarajiwa kufanya mazungumzo na maofisa wa Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) wakiongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Daniel Yohanes. 

Tanzania ni miongoni mwa wafaidikaji wakuu wa mpango huo wa Serikali ya Marekani ikiwa imepatiwa Dola za Marekani milioni 698. 

Tanzania itakuwa inawania kufanya majadiliano kwa ajili ya hatua ya pili ya kupewa fedha za maendeleo. 

Ni miongoni mwa nchi zinazopigiwa mfano na Marekani miongoni mwa nchi zinazoendelea. Marekani imeeleza mara kadhaa kuvutiwa na jinsi Rais Kikwete alivyofanikisha mafanikio ya Serikali yake. 

MCC imevutiwa na Rais Kikwete kwa hatua zake za kupunguza umasikini, kuimarisha usalama wa chakula na kutoa fursa za kiuchumi, kuwa miongoni mwa mabadiliko ya kuongezeka kwa uwazi, utawala bora na maendeleo nchini.



Habari Leo

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts