Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » UZINDUZI WA UTOAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA WASITISHWA

UZINDUZI WA UTOAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA WASITISHWA

Written By mpekuaji on Monday, May 14, 2012 | 8:38:00 PM

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya vitambulisho vya Taifa Bw.Dickson Maimu Akiongea na wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari waandamizi leo makao makuu ya mamlaka ya vitambulisho vya Taifa jijini Dar es salaam, kuhusu kusitishwa kwa muda wa uzinduzi wa utoaji vitambulisho vya Taifa uliokuwa ufanyike mapema mwezi huu, ili  kuyafanyia kazi mapendekezo ya wadau yaweze kuingia kwenye mfumo.
 
Hata Hivyo Bw.Dickson Maimu amesema mradi umekamilika ila zimejitokeza changamoto na mahitaji ya msingi kutoka kwa wadau muhimu wa vitambulisho vya Taifa kwa hiyo mamlaka haina budi kuyafanyia kazi ili kitambulisho kiwe kimekidhi maitaji yote ya msingi.
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo leo katika makao makuu ya mamlaka ya vitambulisho vya taifa jijini Dar es salaam.
Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts