Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » MTOTO ALIYEZALIWA NA VICHWA VIWILI AFARIKI

MTOTO ALIYEZALIWA NA VICHWA VIWILI AFARIKI

Written By mpekuaji on Friday, June 8, 2012 | 12:29:00 PM

Mtoto wa ajabu mwenye vichwa viwili

Mtoto wa ajabu mwenye vichwa viwili aliyezaliwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili MNH), amefariki baada ya kuishi kwa siku moja na nusu.

Afisa Uhusiano Msaidizi wa MNH, Jezza Waziri, alisema mtoto huyo alifariki juzi majira ya saa 12:00 alfajiri akiwa katika matayarisho ya kufanyiwa uchunguzi.

Waziri alisema mtoto huyo alikuwa na jinsia ya kike. Hata hivyo, Waziri hakuwa tayari kutaja jina la mwanamke aliyejifungua mtoto huyo kwa maelezo kwamba kumtaja jina atakuwa anakwenda kinyume cha utaratibu wa kitabibu.

“Hatuwezi kutaja jina la mwanamke kwa sababu hatutaweza kumtendea haki, pia maadili yetu hayaturuhusu isipokuwa kwa ruhusa maalum,” alisema.

Hata hivyo, habari zinasema kuwa mama yake ni mkazi wa Mbagala mwenye umri wa miaka 20 (jina tunalihifadhi). Chanzo cha kifo chake hakijafahamika na madaktari wanaendelea kufanya uchunguzi.
 
CHANZO: NIPASHE

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts