Ni ukweli ulio wazi kuwa Prezzo ana nafasi kubwa zaidi ya kuibuka mshindi wa Big Brother Africa Stargame.
Kwa matumaini hayo Jaguar aliyekuwa akimkebehi Prezzo kuwa yuko broke sasa hivi ajiandae na ujio mpya wa mfalme huyo wa pamba.
Kwa mujibu wa kura zilizopigwa kwenye tovuti rasmi ya Big Brother Africa Stargame, kumchagua nanu atakuwa mshindi, Prezzo ameongoza kwa kupata asilimua 43 ya kura.
Nafasi ya pili imekatwa kwa mbali na Lady May mwenye 17.3%, Keagan 16.3% , Talia 9.7% na Wati 3.0%.
Mshiriki wa Uganda Kyle mambo yake ni magumu zaidi labda kama wananchi a Uganda wakiongeza nguvu ya kupiga kura.
Post your Comment


