Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » ASAH MWAMBENE ATEULIWA KUWA MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI MAELEZO

ASAH MWAMBENE ATEULIWA KUWA MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI MAELEZO

Written By mpekuaji on Wednesday, August 1, 2012 | 2:24:00 PM


     Bw. Asah Andrew Mwambene ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuanzia tarehe 01 Julai, 2012.  Bw. Mwambene anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Clement Mshana ambaye mwaka jana aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Bw. Mwambene (41) kabla ya uteuzi huu alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Aidha, Bw. Mwambene amewahi kufanya kazi katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) akiwa mwakilishi wa Kampuni hiyo huko Zanzibar.

Idara ya Habari (MAELEZO) ndiyo Msemaji Mkuu wa Serikali hapa nchini.


IMETOLEWA NA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI
   NA MICHEZO

AGOSTI 1, 2012

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts