Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » JOSE CHAMELEONE AANZISHA KUNDI LA MAENDELEO LIITWALO MOTO MOTO

JOSE CHAMELEONE AANZISHA KUNDI LA MAENDELEO LIITWALO MOTO MOTO

Written By mpekuaji on Monday, August 13, 2012 | 6:46:00 PM



Mwanamuziki wa Uganda  Jose Chameleone ameanzisha kundi la shughuli za maendeleo liitwalo Moto Moto.

Amesema kundi hilo halitajihusisha na siasa bali kufanya kazi ya kuwahimiza wananchi wa Uganda kufanya kazi na kuchangia shughuli za maendeleo pamoja na kuachana na tabia ya kufanyiwa kila kitu na serikali.

Amesema ameshaachia wimbo wenye jina hilo ili kusaidia kupigia debe shughuli za kundi hilo.

“Maisha yetu yapo mikononi mwetu, naishi kwenye nchi hii na naona kinachotokea mbele yangu. Mimi sio kipofu wa kushindwa kuona ongezeko la bei ya mafuta ya kupikia, sukari, ada za shule na vingine.

  Naona watu wakihitimu Makerere na shahada bila kazi, nasikia watu wakilalamika kuhusu serikali na wabunge hawafanyi kwaajili yetu, lakini tunahitaji kuacha kulalamika na kutafuta mabadiliko tuyatakayo", aliuambia mtandao mmoja wa Uganda.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts