
| Rita Paulsen |
Mitandao ya kijamii hususan Facebook na Twitter, huonesha kirahisi namna watu maarufu wanavyokubalika zaidi kwa mashabiki.
Kuna nyota wengi Tanzania ambao pamoja na umaarufu wao mkubwa hawana ushawishi wowote kwa mashabiki wanaowafuata Twitter au kulike page zao za Facebook.
Usishangae unapoona nyota ana mashabiki zaidi ya 20,000 Facebook lakini aandikapo kitu comments hazizidi 100. Unadhani kwanini iko hivyo? Ni kutokana na jinsi mtu huyo alivyo na ushawishi mkubwa.
Kwa Utafiti tuliyoifanya Facebook, tumebaini kuwa katika nyota wa Tanzania ama watu watu maarufu ukiachana na wale waliopo kwenye siasa, Rita Paulsen aka Madam Rita wa BSS, ndio mwanamke, nyota wa Tanzania mwenye ushawishi mkubwa kuliko wote Tanzania. Je! ni kwasababu ya uzuri wake?
Chochote aandikacho, hata kama ni cha kawaida tu, hupata maoni mengi tofauti na status za watu wengi kwenye kurasa za Facebook ambao wanamzidi hata idadi ya mashabiki waliolike page zao.
Anafuatiwa na Lady Jaydee na Fid Q. Huu ni mfano wa status zao na jinsi zinavyochangiwa.
Madam Rita
19.08.2012
Nawatakia mashabiki wangu wote Eid njema. Eid Mubarak!
Comments – 218, likes 413
21.08.2012
Ahsanteni sana kwa support mlionionyesha na mnayo endelea kunionyesha kipindi hiki cha matatizo. Nawatakieni siku njema.
Comments – 425, likes 644
24.08.2012
Hamna utajiri mkubwa duniani kama afya yako. Nawatakia Ijumaa njema.
Comments 178, Likes 429
Lady Jaydee

Julai 21, 2012
Good morning, kuna siku ningependa nikutane na wote nyie mlioko humu ndani ila sijui nitafanyaje, na itakuwaje?? Mko kama 14,953 au ningoje mfike 15,000 tukutane kwa namba ya 100 mia?? Let me know
Comments 228, likes 333
Julai 30
STATUS zangu hazihusiani na STORY za magazeti, poleni kwa mlioelewa vibaya ila ni mgongano wa mawazo, kuna mtu kanifanyia kitu mimi halafu anaogopa Gardner atamnywesha sumu na hii ilikua maalum kwa ajili yake, kwanza sisomagi magazeti ya aina hiyo ndio maana sikua naelewa hata mnaongelea nini... Ieleweke hivyo, mimi sio MUNGU wala sina haki ya kuhukumu bila uhakika
Comments 156, likes 221
Agosti 1
Captain G Habash anarudi Radio. Atasikika kuanzia September 1, 2012...Stay tuned, kujuaa jina la kipindi na Radio gani !!!
Comments 148, likes 280
Fid Q

Agosti 18
Eid Mubarak to ya all......... Love always!!!!
Comments 158, likes 433
Agosti 17
Leo kwenye Fidstyle Friday tutapelekwa Mwanza kuona mauaji ya 'Young Killah a k a Lil K' kuanzia saa tatu na nusu ya usiku huu ndani ya EATV pekee..!! JOIN THE REVOLUTION
Comments 129, likes 221
Post your Comment


