Get the latest updates from us for free

mas template
Home » , , , , » KUFURU: WEMA SEPETU AMUOGESHA MREMBO KWA POMBE KALI

KUFURU: WEMA SEPETU AMUOGESHA MREMBO KWA POMBE KALI

Written By mpekuaji on Monday, October 22, 2012 | 10:06:00 AM


KATIKA kuonesha jeuri ya fedha, Wema Isaac Sepetu amefanya kufuru kama kawaida yake baada ya kumlowanisha mwili mzima kwa pombe za bei mbaya mrembo aitwaye Rehema Kimbu.


Mrembo Wema Sepetu akimwogesha Rehema Kimbu kwa pombe.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri nyumbani kwa mwigizaji Aunt Ezekiel, Mwananyamala, Dar, Ijumaa iliyopita ambapo Wema na Aunt walimfanyia ‘sapraizi’ ya birthday  Rehema ambaye ilikuwa siku yake ya kuzaliwa.

Katika hali ya kushangaza, Rehema ambaye ni shosti mkubwa wa Aunt alishtukia anamwagiwa pombe mfululizo aina ya Gordon’s na Jack Daniels huku mwigizaji Nice Chande akimmiminia chupa kubwa kadhaa za maji.

Muda mwingi Wema alikuwa akimmwagia Rehema pombe bila kushusha mkono. Kufuatia kitendo hicho kilichoambatana na kelele nyingi za mastaa hao,  kilisababisha wapita njia kujazana getini kwa Aunt bila kujua kilichokuwa kikiendelea na kudhani Rehema alikuwa akipokea kipigo.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts