Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » SKENDO CHAFU ZAMTOA MACHOZI MONALISA

SKENDO CHAFU ZAMTOA MACHOZI MONALISA

Written By mpekuaji on Tuesday, October 9, 2012 | 5:18:00 PM


MSANII nguli anayefanya vizuri kwenye tasnia ya filamu bongo Monalisa, amefunguka na kudai kuwa huwa anatokwa na machozi pale anapoona wasanii wengine wa tasnia hiyo wanafanya mambo ambayo yanaipelekea fani hiyo kuonekana ya kihuni.

Msanii huyo unaweza kusema ni moja kati ya nyota wanaofanya filamu za viwango vya kimataifa, na ndiyo maana ameweza kufika mbali ikiwemo kuingizwa kwenye tuzo kubwa kubwa za kimataifa.


Monalisa
alisema kuwa mara nyingi huwa anashindwa kuelewa ni kitu gani kinachosababisha msanii kufanya mambo ya ajabu badala ya kutulia na kubuni vitu vya kufanya kwa faida ya taifa na tasnia kwa ujumla, wasanii wa nje wanapata umaarufu kupitia kazi zao ambazo zinadumu sokoni kwa muda mrefu kutokana na umakini wao.

“Kila msanii anajua anafanya nini kwenye tasnia hii lakini wote kwa pamoja lazima tujue kwamba hakuna filamu ambayo tunaweza kusema imetikisa dunia kutoka Tanzania, hivyo tunajukumu kubwa la kubuni vitu ili nchi yetu ifike mbali kupitia filamu, lakini wasanii wetu hawafikilia kitu kama hicho,”
alidai.

Aliongeza kuwa kuna mitazamo feki ndani ya tasnia hiyo kuwa msanii hawezi kuwa maarufu bila skendo ambapo kwa upande wake anaamini hiyo haina maana kwa kikubwa kinachoweza kumtangaza msanii ni kufanya kwa nzuri.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts