Akizungumza na Mwandishi wetu, mmoja wa ndugu wa mwanaume aliyeomba jina lake lisiandikwe mtandaoni alisema, wawili hao waliachana hivi karibuni baada ya kuona ndoa yao ‘inanyevuliwa’.
“Ni kweli wameshindwana na sasa kila mmoja yuko kivyake,” alisema ndugu huyo.
Sandra alipotafutwa kuzungumzia hilo hakuwa tayari kutoa ushirikiano, mumewe hakuweza kupatikana ila mdogo wa mume ambaye ni Miss Tanzania 2012, Salha Israel alikiri ndoa ya kaka yake kusambaratika.
Post your Comment