” Hata mambo yanavyoenda nafikiri wewe mwenyewe unaona na kuna vitu pia nimeviona na kuna watu pia nimewaona, unajua adui sio mtu wa kumsahau hata kama hauna kinyongo nae lakini usimsahau kwamba ni adui”LORD EYEZ
Baada ya kuyasema hayo Lord Eyes ambae yuko nje kwa dhamana baada ya kushikiliwa na polisi kwa zaidi ya siku 10 kutokana na tuhuma za wizi wa vifaa vya gari la msanii Ommy Dimpoz hakutaka kuendelea tena kuzungumza ila hiyo ndio msg fupi aliyotaka kuizungumza.
Mpaka sasa amesema ni nyimbo tatu alizonazo kichwani zenye mistari kuhusu kilichomkuta kwenye tuhuma hizo za wizi ambazo atazitoa na kuna uwezekano moja akaitoa december hii.
Post your Comment



