Ni kutokana na kifo cha Robert Karamagi (27) aliyefariki katika Hospitali ya Mulago baada ya majeraha aliyoyapata nyumbani kwa mwanamuziki huyo huko Seguku Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kajjansi Ibrahim Saiga alisema wamechukua ushahidi mbalimbali kutoka kwa majirani na mashuhuda walioona, ushahidi ambao unapingana na ule uliotolewa na familia ya Mayanja.
Pamoja na kusema faili la uchunguzi huo litapelekwa kwa Mwendesha Mashitaka wa Serikali (DPP) kwa ushauri, Saiga alisema pia baba wa Karamagi alikana kwamba mwanaye alijimwagia mafuta na kujiwasha moto, pia alisema mwanaye alipomwita hospitalini alimwambia aliteswa, akafungwa kamba, akamwagiwa mafuta na kuchomwa moto na mwanamuziki huyo pamoja na wenzake wa kundi lake.
Jose Chameleone akihojiwa na NTV Uganda na kusema kwamba hilo swala wameliacha kwenye mikono ya polisi, gazeti la sunday mail limeripoti pia kwamba alhamisi iliyopita Jose Chameleone alihojiwa na wapelelezi kwa muda mrefu lakini aliachiwa kwa dhamana.
Video ya Taarifa ya habari
Post your Comment



