CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimekishukia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) kwa hatua zao za kutaka kwenda kuishitaki serikali
kwa wananchi juu ya hatua, ambazo zimekuwa ikichukua za kuziba mianya ya
rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.
Kimesema ni lazima watu wahoji kama Rais John Magufuli, anafanya
mambo yenye maslahi mapana kwa taifa lakini Chadema inadai ni udikteta,
kinafanya hivyo kwa maslahi ya nani, kimetumwa na nani na kinafadhiliwa
na nani.
Hayo yalielezwa jana na Msemaji wa Chama hicho, Christopher ole
Sendeka wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo za
Makao Makuu ya Chama hicho zilizopo Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam.
Alisema ni jambo la ajabu kuona wakati serikali inashughulika na
walanguzi wachache, ambao wamekuwa wakilikosesha taifa mapato, kikundi
cha watu wachache wanaenda kukisemea kikundi hicho na kuitaja Tanzania
kama nchi ya kifashisti na kidikteta jambo ambalo si sawa.
Post your Comment



