Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja
amewataka mashabiki katika mitandao ya kijamii kuacha kuandika maneno ya
kumbeza Diamond Platnumz baada ya kukosa tuzo ya BET na kuchukuliwa na
Black Coffee kutoka Afrika Kusini.
Rapper huyo ambaye ameachia remix ya wimbo ‘My Life’ hivi karibuni
akiwa amemshirikisha Radio & Weasel kutoka Uganda, ameiambia Bongo5
kuwa hatua aliyoifikia Diamond kimataifa ni kubwa hivyo anapaswa
kupongezwa.
“Unajua watu walikuwa wanamatarajio makubwa sana na tuzo lakini
mwisho wa siku tukubali matokeo ya kushinda na kushindwa,” alisema Dogo
Janja.
Aliongeza, “Diamond bado ni mshindi, alikuwa mtanzania pekee, kwa
hiyo huu sio wakati wakumbeza, tumtie moyo ili aendelee kupambana
zaidi,”
Diamond ni msanii pekee wa Tanzania ambaye alikuwa kwenye
kinyang’anyiro cha tuzo hiyo ambayo ilichukuliwa na msanii kutoka Afrika
Kusini.
Post your Comment



