Mahakama
ya Rufani Tanzania, imeamuru jalada la kesi inayomkabili Kamishna Mkuu
wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake
kurudishwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikilizwa rufani ya Jamhuri.
Pia,
imeagiza jalada hilo lipangiwe kusikilizwa kwa jaji mwingine dhidi ya
rufaa ya kupinga kuondolewa shtaka la utakatishaji fedha katika kesi ya
kujipatia Dola za Marekani milioni 6.
Hukumu
hiyo ilisomwa juzi na Msajili wa Mahakakama ya Rufani, Zahra Maruma
baada ya kusikilizwa na jopo la majaji watatu, likiongozwa na Mwenyekiti
Salum Masati akisaidiana na Kipenka Musa na Augustine Mwarija.
Msajili
Maruma alisema mahakama hiyo imeona kwamba Jaji Mfawidhi Moses Mzuna
alikosea kukubali pingamizi la utetezi na kutupilia mbali kusikiliza
rufani ya kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
wa kuliondoa shtaka la kutakatisha fedha dhidi ya Kitilya na wenzake.
“Mahakama
hii imebatilisha uamuzi uliotolewa na Jaji Mzuna na kwamba imeamuru
jalada lirudishwe Mahakama Kuu kwa ajili ya kupangiwa jaji mwingine wa
kusikiliza rufani ya upande wa Jamhuri kuhusu kuondolewa kwa shtaka
hilo” alisema Msajili na kuongeza.
“Kwa
kuondolewa shtaka hilo Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) hakuwa na
namna ya kurudi Mahakama ya Kisutu kuomba kufanya mabadiliko ya hati ya
mashtaka kwa sababu kila shtaka linajitegemea na kwamba shtaka la
kutakatisha fedha lilishaondolewa na kumalizika katika hati hiyo ya
mashtaka dhidi ya washtakiwa” alisema Msajili Maruma wakati akisoma hukumu hiyo.
Akifafanua
zaidi alisema Mahakama ya Rufani imebatilisha uamuzi uliotolewa na
Mahakama Kuu na kuamuru kusikilizwa rufani ya DPP kama ilivokuwa
imekatwa.
Mapema
Mei 31, mwaka huu upande wa Jamhuri ukiongozwa na DPP, Biswalo Mganga,
Naibu DPP, Osward Tibabyekomya, Mawakili wa Serikali Waandamizi,
Shadrack Kimaro na Awamu Mbagwa uliomba mahakama hiyo kuangalia uhalali
wa kuondolewa shtaka la kutakatisha fedha pamoja na uamuzi wa Jaji Mzuna
kutupilia mbali rufani yao.
“Watukufu
Majaji ni rai yetu upande wa Jamhuri, tunaomba mahakama hii iangalie
upya na kuiamuru Mahakama Kuu kusikiliza rufaa ya kuliondoa shtaka la
kutakatisha fedha …”alidai DPP Mganga.
Akiwasilisha
hoja za rufaa hiyo mahakamani hapo, Tibabyekomya alidai kuwa malalamiko
yao ni kwamba Jaji Mfawidhi, Mosses Mzuna alikosea kukataa kusikiliza
rufaa ya kuondolewa kwa shtaka hilo na mahakama ya chini.
Alidai kuwa kinachashtakiwa katika shtaka ni kosa ambalo limekamilika na kwamba linasisimama kwa kujitegemea.
“Watukufu
majaji kitendo cha kufuta kabisa shtaka la nane la kutakatisha fedha
dhidi ya washtakiwa kulihitimisha shtaka hilo kama lilivyokua
limeshtakiwa kwa kuwa lilikuwa linajitegema”alidai na kuongeza kuwa.
“Jaji
Mzuna alikataa kwamba mahakama yake haina uwezo wa kuruhusu kufanya
mabadiliko ya hati ya mashtaka na kwamba uamuzi huo ulionyesha
haiwezekani kufanyika mabadiliko amri ambayo inahitimisha shtaka la
nane” alidai msaidizi huyo wa DPP.
Mawakili
wa utetezi wakijibu hoja za Jamhuri kwa nyakati tofauti; Wakili Majura
Magafu alidai kuwa rufaa hiyo haina mashiko ya kisheria na kwamba
ilifunguliwa mapema kinyume cha sheria mahakama hiyo itupilie mbali.
“Hakimu
Mchauru hakukosea kama inavyodaiwa na Jamhuri kwa sababu alitoa nafasi
kwamba wakati utakapofika kisheria wataruhusiwa kufanya mabadiliko… “alidai Magafu.
Dk.
Ringo Tenga alidai kuwa baada ya kuondolewa shtaka hilo, upande wa
Jamhuri haukuwasilisha maombi ya kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka.
Alex
Mgongolwa alidai kuwa hoja zao za utetezi kwamba rufaa hiyo haina
sababu za kutosholeza kisheria imefunguliwa kinyume cha sheria mahakama
ifutilie mbali.
Mbali
na Kitilya, washtakiwa wengine ni, aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 1996,
Shose Sinare na mwanasheria wa benki ya Stanbic Tanzania, Sioi Solomon.
Post your Comment



