Serikali
ya Tanzania imebadilisha mfumo wa maadhimisho ya siku ya utumishi wa
umma badala yake siku hiyo ya tarehe 16 hadi 23 mwezi huu itatumika kwa
watendaji wakuu wa wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala na taasisi za
serikali kusikiliza kero za watumishi wa umma katika maeneo yao ya kazi
kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mh. Angellah
Kairuki amesema hakutakuwa na maonesho katika viwanja vya Mnazi Mmoja
kama ilivyozoeleka kwani bado kuna changamoto nyingi zinazowakabili
wafanyakazi na hivyo vyema siku hiyo wakasilizwa ili kutatuliwa.
Aidha katika hatua nyingine waziri Kairuki amesema kuanzia tarehe 1
Machi mwaka huu hadi tarehe 30 mwezi Mei mwaka huu jumla ya watumishi
12,246 wameondolewa kwenye mfumo wa malipo ya miashahara kwa sababu
mbalimbali zikiwemo za kutimiza umri wa kustaafu kwa lazima, kufariki au
kufukuzwa kazi.
Amesema katika zoezi hilo pia jumla ya shilingi 25,091,292,688,82
zingepotea kama watumishi wasingeondolewa kwenye mfumo ikilinganishwa
watumishi 10,295 walioondolewa kwenye mfumo hadi tarehe 30 Aprili mwaka
huu na jumla ya shilingi 23,206,547,598.82 zilizookolewa ambapo hilo ni
ongezeko la watumishi 1,951 na shilingi 1,884,745,090.
Post your Comment



