Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa
akionesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mfumo wa ufatiliaji wa
kielektroniki katika jengo la kituo cha kutunza taarifa mbalimbali (data
centre) kitakachoanza kazi rasmi mwezi Aprili mwaka huu jijini Dar es
Salaam. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka sekta ya Mawasiliano
Eng. Peter Mwasalyanda.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa
akitizama kwa karibu mtambo wa kuratibu usalama katika kituo cha kutunza
taarifa mbalimbali (data centre) jijini Dar es Salaam. Kituo hicho cha
kwanza kujengwa nchini kitatunza taarifa za Serikali na sekta binafsi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa
akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka sekta ya Mawasiliano
Eng. Peter Mwasalyanda wakati akikagua kituo cha kutunza taarifa
mbalimbali (data centre) kitakachoanza kazi rasmi mwezi Aprili jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo kwa
Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka sekta ya Mawasiliano Eng. Peter Mwasalyanda
wakati akikagua kituo hicho cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre)
kitakachoanza kazi rasmi mwezi Aprili jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amezitaka taasisi za Serikali na
binafsi kukitumia kituo cha kisasa cha kuhifadhi taarifa (data centre)
kutunza taarifa zao ili kuzihakikishia usalama na uhakika wa kuzitumia
wakati wote.
Akizungumza baada ya kukagua
kituo hicho kinachosimamiwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
sekta ya Mawasiliano amesema asilimia 75 imetengwa kwa ajili ya kutunza
taarifa kutoka sekta binafsi na asilimia 25 itatunza taarifa za
Serikali.
Waziri Mbarawa amezitaka taasisi
za Benki, Simu, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Wakala wa Serikali
Mtandao (e-GA) kutembelea kituo hicho kujifunza mifumo ya uhifadhi
taarifa na kujiunga ili kunufaika na huduma za kituo hicho.
Amesema huduma ya mtandao katika
kituo hicho imeimarishwa kutokana na kuunganishwa na mkongo wa taifa na
hivyo itawarahisishia wateja wake kuweka na kuchukua taarifa kwa haraka.
Kituo hicho ambacho ni cha kwanza
kujengwa katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ni fursa
mpya kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali wenye taarifa nyingi
kuzihifadhi na kuzitumia wanapozihitaji kinalimikiwa na Serikali.
Post your Comment






