Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli
amefuta hati ya mashamba ya Mkonge, yenye hekta zaidi ya 5,000
yaliyokuwa yametelekezwa na kuwa mapori ambayo hayaendelezwi kufuatia
malalamiko ya wakazi zaidi ya 2,000 wa kijiji cha Kibaranga kuhangaikia
maeneo ya kilimo na kusababisha migogoro ya mara kwa mara baina yao.
Akizungumza
na wananchi wa kijiji cha Kibaranga katika mkutano wa hadhara, Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi
amesema hili ni shamba la sita kufutwa na kuwapa wananchi na Mheshimiwa
Rais katika wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga kufuatia wawekezaji waliopewa
hati ya kuyaendeleza kushindwa kutekeleza makubalino.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella amesema Serikali ya
mkoa wa Tanga imepewa jukumu la kugawa ardhi hiyo na watahakikisha kuwa
wanaweka utaratibu utakaowezesha kila mwananchi apate shamba na hati ili
yaweze kuwaendeleza wananchi.
Kufuatia
hatua hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia ulinzi na
usalama Mheshimiwa Adadi Rajab amesema watahakikisha wawekezaji matapeli
hawaruhusiwi kujimegea ardhi kwa manufaa yao na badala yake mashamba
hayo yaendelezwe na wananchi waliokabidhiwa ili yaweze kuwapa manufaa.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akiwatangazia
wanakijiji wa Kibaranga kuwaelezea uamuzi wa Rais Dk John Pombe Magufuli
wa kufuta hati ya Shamba leyenye hekta zaidi ya 5,000 ambalo lililokuwa limetelekezwa na mwekezaji, kwenye kijiji cha Kibaranga kilichopo wilayani Muheza mkoani Tanga.
Mhe.
Lukuvi akiwapa muongozo wanakijiji wa Kibaranga jinsi ya kugawana
shamba hilo ambalo limerejeshwa kwao na Mhe. Rais baada ya kufuta hati
ya Shamba hilo kwenye kijiji cha Kibaranga kilichopo wilayani Muheza
mkoani Tanga.
Wakazi wa kijiji cha Kibaranga wakielezea furaha yao kwa Mhe. Lukuvi kwa uamuzi wa Rais Dk John Pombe Magufuli kufuta hati ya Shamba lililokuwa limetelekezwa na mwekezaji kwa muda mrefu.
Mbunge
wa Jimbo la Muheza mkoani Tanga kilipo kijiji cha Kibaranga, Mhe. Adadi
Rajabu akizungumza baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, William Lukuvi kuwaelezea wanakijiji hao uamuzi wa Rais Dk John
Pombe Magufuli kufuta hati ya Shamba lililokuwa limetelekezwa na
mwekezaji, kwenye kijiji cha Kibaranga kilichopo wilayani Muheza mkoani
Tanga.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na
viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza muda mfupi baada ya kuwasili
wilayani humo akitokea Lushoto, Tanga kabla ya kuelekea Kijiji cha
Kibaranga kufuta hati ya Shamba lililokuwa limetelekezwa na mwekezaji.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza muda mfupi baada ya kuwasili wilayani humo akitokea Lushoto, Tanga kabla ya kuelekea Kijiji cha Kibaranga kufuta hati ya Shamba lililokuwa limetelekezwa na mwekezaji.
Post your Comment









