Ukosefu wa Lift katika jengo la wagonjwa la taasisi ya mifupa ya MOI
katika Hospitali kuu ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam umeelezwa kuwa
moja ya changamoto kubwa inayowakabili wagonjwa wanaofika katika kitengo
hicho kwa ajili ya kupata matibabu.
Muonekano wa jengo bora na imara la kitengo cha mifupa katika
hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam, ambalo ukosefu wa lift licha
ya kuwa mwiba kwa wagonjwa.
Ambapo mmoja wa wauguzi wa jengo hilo ambaye tunahifadhi jina lake
ameeleza kuwa madhara wanayoyapata kuwapandisha wagonjwa kutoka ghorofa
ya kwanza hadi ya tano kwa kutumia ngazi.
Huku tukipiga picha kwa usiri, tulizungumza na mmoja wa mafundi wa
kampuni ya Premider Elevetor ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake
ambapo amesema wameamua kusitisha utoaji huduma wa Lift kutokana deni
kubwa wanaloidai taasisi hiyo, na kwamba watafanya hivyo mpaka pale deni
lao litakapolipwa.
Lakini uongozi wa taasisi hiyo ya mifupa ya MOI umesisitiza hakuna
tatizo la Lift katika jengo hilo,huku wagonjwa wakisema Lift ni
changamoto kuu kwa wiki sita sasa.
Post your Comment



