Msajili Msaidizi wa Vyama vya
Siasa Upande wa Uhakiki wa Vyama vya Siasa Bwana. Sisty Nyahoza ameanza
zoezi la kuhakiki utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya
Sheria ya Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam leo.
Bw.Willy Brown Nyantiga,
Mhasibu kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini akihoji
taarifa za fedha wakati wa zoezi la kuhakiki utekelezaji wa masharti ya
usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa kwa chama cha NLD Jijini
Dar es Salaam leo . Katikati ni Mwenyekiti wa chama , Bw. Oscar
Emmanuel Makaidi na Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Tozzy Ephraim
Matwanga ( kulia)
Msajili Msaidizi wa Vyama vya
Siasa Upande wa Uhakiki wa vyama vya Siasa , Bw. Sisty Nyahoza (kulia)
akihakiki daftari lenye orodha ya wanachama wa Chama cha National League
for Democratic (NLD) wakati wa zoezi la kuhakiki wa utekelezaji wa
masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa leo Jijini
Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa chama hicho Oscar
Emmanuel Makaidi na Katibu Mkuu wa NLD Tozzy Ephraim Matwanga.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya
Siasa Ibrahim Mkwawa (wa kwanza kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama cha Sauti ya Umma
(SAU) wakati wa zoezi la kuhakiki utekelezaji wa masharti ya usajili na
matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam leo.
Post your Comment






