MUIGIZAJI mkongwe kwenye Tasnia ya Filamu Bongo, Fatuma Makongoro ‘Bi
Mwenda’ amefunguka kuwa anaona uzee umeshamfikia hivyo muda si mrefu
ataamua kupumzika kuigiza ili afanye kitu kingine kulingana na umri
wake.
Akizungumza nasi, Bi Mwenda alisema amecheza filamu muda
mrefu takriban miaka ishirini hivyo anaona wazi atashindwa kukimbizana
kwenye kambi kwenda huku na huko kutokana na umri wake hivyo anajipanga
kuangalia afanye nini.
“Kweli kabisa nikijiangalia uzee umeshagonga hodi na siwezi kuukimbia
ila kwa sasa najipanga nipumzike kwani ni muda mrefu niko kwenye sanaa,
nitaangalia nifanye nini ili kipato changu kiendelee,” alisema Bi
Mwenda pasipo kuainisha atasimama baada ya muda gani.
Post your Comment



