Ubuyu ulionyooka mjini kwa sasa unamgusa staa wa sinema za Kibongo,
Shamsa Ford ‘Chausiku’ anayedaiwa kujitwalia mwanaume aitwaye Chid
Mapenzi huku nyuma yake kukiwa na mazito kwamba, mwanaume huyo aliwahi
kumilikiwa na mwigizaji Jacqueline Wolper Massawe ‘Gambe’.
Kumekuwa na habari za chini kwa chini kuwa Shamsa anatoka na Chid
Mapenzi ambaye ni mfanyabishara wa jijini Dar ambapo hivi karibuni,
mwanamama huyo alitupia picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na
mwanaume huyo.
Katika picha hizo ambazo chanzo cha uhakika kinashikilia ‘nakala’ zake, Shamsa
anaonekana akijiachia na Chid Mapenzi huku akiwa amemziba sura.
Ilidaiwa kwamba, bidada huyo alidhani watu hawatamtambua jamaa huyo
lakini ‘watu wabaya kwa ubuyu’ ambao wanamjua vizuri Chid Mapenzi,
hawakusita kuchukua hatua kwani ndani ya dakika sifuri walitupia jina
lake na picha za tatuu yake kuonesha ushahidi kuwa ni yeye.
Baada ya kutajwa kwa jina hilo ndipo yakaibuka maneno mengi ikiwa ni
pamoja na kejeli za kumsema Shamsa kuwa ‘amepotea’ kwa mwanaume huyo
kwani alishakuwa na uhusiano wa kupika na kupakua na Wolper.
Kama kawaida, Mwandishi wa Ubuyu alifuatilia sakata hilo hatua kwa
hatua ili kubaini ukweli kama Wolper aliwahi kutoka na Chid Mapenzi.
Katika ufukunyuzi wa hali ya juu, ilibainika kwamba, kuna
ukweli ambao ulipatikana kupitia marafiki wa karibu wa Wolper.
Huku akiomba hifadhi ya jina, mmoja wa marafiki hao wa
Wolper alimhakikishia mwanahabari wetu kuwa hakuna shaka kwamba Wolper
alishakuwa mtu wa Chid Mapenzi lakini ni kitambo kidogo.
“Ni kweli hata yeye (Wolper) hawezi kubisha kwa sababu amekuwa na Chid japokuwa ni zamani kidogo.
“Wapo wanaosema walimwagana lakini wakarudiana kisha wakaachana tena
ila mimi hilo la kumwagana na kurudiana kisha kumwagana tena sina
uhakika nalo lakini ukweli ni kwamba walikuwa wakipendana mno hadi
wakawa kero kwa baadhi yetu,” kilinyetisha chanzo hicho.
Kama Wolper na Chid walikuwa wapenzi enzi hizo, hilo halimzuii Shamsa
kuwa na uhusiano na mfanyabiashara huyo. Kibaya ingekuwa ni kama Shamsa
angeingilia penzi hilo likiwa hai kwani tujuavyo mwanamke kama
hajaolewa anaweza kuolewa na mwanaume yeyote na pale Mungu alipokupangia
huwezi kupangua.
Ila nawasihi wasanii kuchunguza wanaume kabla ya kuingia nao kwenye
mapenzi ili kuepusha kuhesabiwa idadi ya wanaume kwani Shamsa hajui
sababu za Wolper kuachana na bwana huyo na yeye inawezekana ameingia kwa
lengo la kutafuta ndoa baada ya kuachana na aliyekuwa mchumba’ke,
Dickson Matoke ‘Dick’ aliyezaa naye mtoto wa kiume, Terry.
Post your Comment



