Kuna tetesi nyingi sana zimevuma kwenye mitandao ya kijamii wiki hii
kuhusiana na Diamond na Zari. Miongoni mwa tetesi hizo ni pamoja na kuwa
Zari haelewani kabisa na ndugu zake Diamond akiwemo mama mkwe wake na
wifi yake, Esma.
Hilo Zari alilielezea kwa mafumbo kwenye Snaochat na kudai kuwa hajali kama nchini au ukoo usipomkubali, ilimradi tu wanapendana na mpenzi wake.
Tetesi nyingine ni kuwa staa huyo wa ‘Utanipenda’ si mwaminifu kwenye
uhusiano wao na kwamba huenda akawa na ukaribu usio wa kawaida na
Hamisa Mobetto.
Yote hayo yanaonesha kuwa si kitu kwenye couple hii na wameamua
kuonesha kuwa wapo strong kupitia Instagram. Wamepost picha na video
kadhaa wakiwa na mtoto wao Tiffah kuashiria kuwa mambo ni shwari.
“Sending love from the other side from me and mines. Have a blessed week,” ameandika Zari kwenye post moja wapo.
Naye Diamond akiwa na familia yake hiyo ameandika, “Aint nothing
better than spending time with the people that you love from the bottom
of your heart……hata ukiwa kijuso, ukiwa nao kasura kanakuwaga kama
kanapata Uhendisamu kwa mbaaaali kwa furaha.”
Post your Comment


