Uongozi wa WCB umeendelea kumwaga zawadi ya magari kwa wasanii wake na sasa bahati imemuangukia Raymond.
Jana ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa msanii Raymond, uongozi wa WCB
ukaamua kumfanyia sherehe msanii wao huyo kwenye ikulu ya Diamond
iliyopo huko Madale lakini kubwa zaidi ni zawadi ya gari aliyopewa
kwenye sherehe hiyo. Bosi wake, Diamond, ameweka kipande cha video
kinachoonesha msanii huyo akikabidhiwa gari hilo aina ya Rav4 yenye
rangi nyeusi.
Raymond anakuwa msanii wa pili kutoka WCB kukabidhiwa gari na uongozi
huo baada ya mwezi Mei mwaka huu uongozi huo kumkabidhi Harmonize gari
aina ya Mark X yenye rangi nyeusi. Rangi nyeusi imeonekana kutawala WCB
kwani hata Diamond anamiliki BMW X6 yenye rangi nyeusi pia.
Wamebakia wasanii wawili ndani ya kundi hilo ambao bado
hawajakabidhiwa magari swali, je ni nani atakuwa wakwanza kuipata zawadi
hiyo kati ya Queen Darlin na Rich Mavoko?
Post your Comment



