Hivi karibuni, Diamond Platnumz alieleza kuwa album yake ijayo itakuwa
ya kimataifa. Na sasa amefafanua zaidi kwanini itakuwa na hadhi hiyo
kupitia interview aliyofanya Ijumaa hii na Radio Maisha ya Kenya.
“Mwanzo nilikuwa natoa album lakini nilikuwa nafocus tu Tanzania
nikaja nikafocus na East Africa so hapa katikati nilikuwa napigania soko
la kidunia. So baada ya kufanya nyimbo za kidunia, nikimaanisha kwamba
kushirikisha baadhi ya watu, sababu ukisema album yako yote iwe nyumbani
Tanzania inakuwa imekaa kiselfish so lazima ufanye na watu wan chi
tofauti tofauti, Kenya, Nigeria, South Africa unachukua Uganda kidogo,
kutoka hapo unafanya na America, unafanya na Europe. Hata production
pia, producers sometimes unachanganya na videographer hiyo inakuwa ni
international album kwasababu kila nchi mtu ataona ni album yao,”
alisisitiza.
Pia alidai kuwa imemchukua muda kuachia album yake ili kuweza
kulisoma soko la dunia na kwamba cha kwanza alichokifanya ni kuhakikisha
mfumo wa kuuza kidijitali wameuweka vyema.Wikiendi hii staa huyo anatumbuiza mjini Meru.
Post your Comment