Kama huwezi utani basi jiweke mbali na Idris Sultan kwa kuwa ipo siku unaweza kujikuta ukifanya kitu usichokitarajia.
Mchekeshaji huyo ameandika ujumbe wa utani kwa Diamond na Zari kwenye
mtandao wake wa Instagram baada ya hivi karibuni kusambaa kwa taarifa
kuwa First Lady huyo wa WCB alikuta hereni kwenye chumba cha Diamond
ikionekana kuwa alimsaliti na mwanamke mwingine.
“Ndio imeingia na DHL @diamondplatnumz nakupitishia hapo maana
umepoteza control mambo yanamwagika hovyo mara hereni ulizisimamia kama
kangaroo,” ameandika Idris kwenye picha aliyoiweka kwenye mtandao huo.
Hakuishia hapo Idris amempongeza Zari The Bosslady kwa kusherehekea
siku yake ya kuzaliwa kwa kuweka picha ya hereni kwenye mtandao huo na
kuandika ujumbe unaosomeka, “Happy birthday @zarithebosslady .”
Post your Comment