Latifa Mohamed aka Queen Tipha amefunguka baada ya kusambaa mitandaoni
picha za mzazi mwenzake, Ben Pol akionekana wakibusiana na Snura wakati
walipokuwa mkoani Tabora kwa ajili ya tamasha la Fiesta.
Queen Tipha amekiambia kipindi cha Clouds E cha Clouds TV kuwa
hakushtuka baada ya kuona picha hizo kwa kuwa mpenzi wake huyo alikuwa
kazini.
“Nimeamka asubuhi nikaona watu wengi wamenitag, nilichukulia kawaida
kwa sababu ni mtu ambaye ninamuamini na aliniaga kuwa anaenda kazini,”
amesema Queen Tipha.
“Sikuona kama ni kitu cha ajabu kwa kuwa yule ni msanii mwenzake na
rafiki yake pia. Nimechukulia kawaida tofauti na watu wanavyofikiria,”
ameongeza. Queen Tipha aliwahi kuwa mshindi wa pili kwenye Miss Tanzania
2013 na wamefanikiwa kuzaa mtoto mmoja na mpenzi wake Ben Pol.
Post your Comment