Mkali wa wimbo ‘Mboga Saba’ Mr Blue baada ya hivi karibuni alipatwa na
msuko suko wa kuyumba kwa ndoa yake, kutokana na kusambaa kwa tetesi za
kuwasiliana na ex wake Najma Dartan, amesema yuko tayari kumchukulia
hatua za kisheria aliyesababisha ugomvi huo.
Rapper huyo amesema yeye binafsi hakuwasiliana na Naj, isipokuwa
habari hizo zilipoanza alidhani ni kiki inayotengenezwa na Naj pamoja
nampenzi wake Baraka The Prince, ili kuachia wimbo wao wa pamoja.
“Ile habari ilikuwa ya uongo, mwanzoni mi nilihisi Baraka na mchumba
wake Najma watakuwa wameitengeneza kwa ajili ya mambo yao ya kutafuta
kiki, kwa sasabu ilisemekana kuna nyimbo yao wanataka kutoa Baraka na
Najma, kwa hiyo wanatafuta kama kiki kutumia ubavu wangu, nikabahatika
kukutana na Baraka na kumshika mkono, na kumwambia akubali mbele za
watu, akasema hajui hiyo taarifa”, Mr Blue alikiambia kipindi cha Planet
Bongo.
Aliongeza,”Hatua za kisheria lazima zichukuliwe unajua hivi vitu sio
vitu vya kuharibiana, mi sa hivi nishakuwa mtu mzima, siwezi kurudia
matapishi ambayo nishawahi kuyatapika, eti nikampigie Najma sijui niwe
nae, kwa sababu mimi najua mke wa kumuoa najua mwanamke wa kuwa naye
ndio maana nikamchagua mke wangu, na nampenda na amenizalia watoto
wazuri, kwa hiyo siwezi tena kufikiria eti kumpigia Najma, siwezi
kufikiria kugombana na Baraka The Prince, kwanza hatulingani, mi wakati
naanza mziki ye bado yuko shule anasoma, kama ni kweli ni wao japokuwa
Baraka amenithibitishia sio wao, nikijua ni wao lazima nitafute njia ya
kuwashikisha adabu”,
Post your Comment



