Kuanzia wiki iliyopita kumekuwa na tetesi ambazo zinasambaa kwa kasi katika
mitandao ya kijamii zikidai kwamba malkia wa filamu, Wema Sepetu
anatumia Madawa ya kulevya ‘Unga’.
Tetesisi hiyo ambazo sio nzuri kwa mwigizaji huyo pamoja na watu wake
wakaribu, zimeonyesha pia kuwagusa baadhi ya mashabiki wa mwigizaji
huyo ambapo wanalazimika kutafuta ukweli wa tetesi hizo kwa namna
yoyote.
Mmoja kati ya mashabiki wa malkia huyo kupitia mtandao wa instagram,
aliamua kumuuliza meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda kuhusu tuhuma
hizo.
Pia rafiki wa karibu wa malkia huyo wa filamu aitwae Muna, kupitia
mtandao wa Global Publisher amekanusha kumwingiza shosti wake Wema
Sepetu kwenye matumizi ya Madawa ya kulevya kwa kusema madai hayo hayana
ukweli.
Post your Comment




