MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA
“Ankooo”
Soroo akamkumbatia Lee Si, wakatoka nje ya ofisi hizo wakiwa wanatembea kuelekea kwenye moja ya bustani wakaka kwenye moja ya viti.
“Unajua ni sehemu gani alipo Black Shadow?”
Lee Si alimuuliza Soroo, mara baada ya kutoa noti ya dola mia na kumkabidhi, Sa Yon a Shamsa waliweza kumuona Lee Si akiwa na mtoto mmoja, Shamsa alipo jaribu kumkazia macho mtoto huyo akagundua ni Junio, jambo lililo mfanya ashuke kwenye gari na kuanza kukimbia kuelekea kule walipo kaa Soroo na Lee Si
ENDELEA
Shamsa akazidisha kasi, hadi karibu na bustani akasita kidogo kukimbia huku macho yake yote akiwa amemtupia Soroo, Lee Si, alipo muona Shamsa akatamani asimame na akimbie, ila akashindwa na kujikuta akiachia tabasamu pana la kinafki ili mradi asistukiwe mpango wake. Shamsa akaanza kutembea hatua za taratibu hadi sehemu walipo Soroo na Lee Si.Kufanana kwa Soroo na Junio ambaye kwa sasa ni Marehemu, kukamfanya Shamsa kulengwa lengwa na machozi.
Saroo akabaki akimshangaa Shamsa aliye piga magoti mbele yake, hakumjua ni nani aliye kuja. Soroo akamtazama Lee Si kisha akamtazama Shamsa, aliye anza kumshika mkono wake wa kulia. Shamsa akashindwa kujizuia na kujikuta akiangua kilio huku akimkumbatia Soroo, uchungu wa kifo cha Junio ukamrejea upya.
“Wewe nani?”
Soroo alimuuliza Shamsa huku ajijitoa mikononi mwake, Shamsa hakumjibu chochote zaidi ya kulia kwani hadi sauti wamefanana, Sa Yoo alisimama kwa mbali akishuhudia hali nzima inavyo endelea.
“Akooo Lee Si eti huyu ni nani?”
“Ahaa ahaa hu…..uuyu…..”
Lee Si alijing’ata ng’ata, hakujua ajibu nini japo swali alilo ulizwa ni rahisi sana kwake.
“Unaitwa nani mtoto mzuri?”
Shamsa alizungumza huku akijipangusa machozi yake kwa kiganja chake cha mkono wa kushoto.
“Soroo, wewe unaitwa nani?”
“Shamsa”
“Mbona sasa unalia?”
Shamsa akajitahidi kuachia tabasamu pana, kisha viganja vyake taratibu vikaanza kupapasa mashavu yote mawali ya Soroo.
“Nimetokea kukupenda”
“Akoo Lee Si, Shamsa ananipenda kama anti Phidaya”
Lee Si alitingisha kichwa tu, mdomo wake alijikuta ukiwa mzito gafla, hata maneno ambayo alipanga kumshawishi mtoto huyo yote yaliparanganyuka kichwani.
“Unamjua anti Phidaya?”
“Eheee alikuja siku ile kutuletea vyakula na hele hapa, akaniambia amenipenda”
“Ahaa basi mimi pia nianakupenda kutokana anti Phidaya ni mama yangu”
“Ahahaa kweliii?”
“Ndio”
Soroo akajikuta akifurahi sana kusikia maneno ya Shamsa, akamkumbatia tena na kumuomba asimame. Mlezi mmoja wa choa baada ya kuona ujio wa Shamsa, ikamlazimu kufika kwenye bustani hiyo kuuliza ni kitu gani kinacho endelea. Ikabidi Lee Si kuchukua jukumu la kumuelezea Shamsa kwamba ni mtoto wa bosi wake ambaye alikuja naye siku chache zilizo pita.
Mlezi huyo baada ya kusikia habari hiyo, akafurahi sana na kuomba kwenye na Shamsa ofisini kumtambulishwa kwa baadhi ya walezi wa chuo hicho ambao wanamuheshimu sana Phidaya kama mwanamke shujjaa aliye jitolea kuwalea watoto hao. Walezi hao hawakusita kumpa pole Shamsa kwa mama yake kutekwa, kila mmoja alisikitika sana kwa taarifa hiyo kwani wameondokewa mtu muhimu sana kwenye maisha yake.
“Nina imani kwamba atakuwa salama, nahisi watu hao wanahitaji pesa tu”
Shamsa aliwafariji walezi hao, ambao tukio la Phidaya kutekwa liliwagusa kwa kiasi kikubwa sana. Ila mlezi mmoja aakashindwa kustahimili kuuliza kitu amchacho kinamsumbua moyoni mwake.
“Mbona weewe na mama yako mumetokea sana kumpenda Soroo, kuliko watoto wengine?”
“Kusema kweli Soroo amefanana sana na mdogo wangu, mtoto wa mama, alifariki mwaka jana akiwa na miaka sita, ndio maana nilipo muona Soroo kwa mara ya kwanza nilijisikia uchungu sana”
MManeno ya Shamsa yakwafanya baadhi ya wamama walezi kumwagikwa na machozi, japo ni maneno machache ila kila mmoja alitambua uchungu wa kufiwa na mtoto, wakamuangalia Soroo, mbaye muda wote alijiegemeza mapajani mwa Shamsa.
Kitendo cha Shamsa kuingia na Soroo ofisini kwa walezi wa kituo cha kulele watoto, kilimkera sana Lee Si akanyanyuka kwa hasira kwenye benchi alillo kuwa amekalia na kwenda kwenye gari lake huku akimpita Sa Yoo pasipo kumsemesha neon la aina yoyote. Sa Yoo kama kawaida yake akamkata Lee Si jicho moja kali, kisha akatabasamu nakuegemea gari la Phidaya ambalo kwa sasa yeye ndio analitumia. Lee Si aliweza kuona kitendo ambacho Sa Yoo amekifanya, hakuhitaji kujibizana na Sa Yoo, akawasha gari na kuondoka kwa kasi huku akitimua vumbi kuingia barabarani.
***
Majira ya saa mbili usiku, ndege ya dokta Ranjiti ikatua wanja wa ndege jijini Cairo nchini Misri. Phidaya akiongozana na wahudhumu wawili wa ndege wakashuka na kumkuta dokta Ranjiti akiwa anawasubiri pembeni yake akiwa Kim pamona na walinzi wengine wapya watatu.
“Karibu mke wangu”
Dokta Rnjito alizungumza huku akiachia tabasamu pana, akajaribu kumkumbatia Phidaya, ila akamzuia na kuongoza moja kwa moja hadi kwenye gari aina Ranger rover Sport, akaingia na kumsubiria mume wake amfwate. Dokta Ranjiti akaingia kwenye gari akiwa amekasirika.
“Kwa nini umeniaibisha mbele ya wafanyakazi wangu?”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa kufoka akiwa amekazia macho Phidaya, ambaye hakujali ukali huo wa dokta Ranjiti
“Umekuwa jeusi sio?”
“Ehee babuee usinipigi……”
Kofi zito likatua shavuni mwa Phidaya, hadi Kim aliye kaa siti ya mbele ahageuka kungalia kinacho endelea, akamkuta Phidaya akiwa amejikunyata huku mikono yake miwili akiiweka kweye shavu alilo tandikwa kofi zito
“Endesha gari”
Dokta Kim alizungumza huku akijiweka vizuri kwenye siti, Kim bila pingamizi akawasha gari na safari ya kueleka kwenye hoteli moja ya kifahari, ambayo dokta Kim, amepangishwa kwa miezi sita ikaanza. Ukimya ndani ya gari ulitawala kwa asilimia mia moja, hapakuwa na mtu aliye zungumza kitu cha aina yoyote hadi wanafika hotelini. Taratibu Phidaya akashuka kwenye gari, baada ya kufunguliwa mlango na Kim, dokta Ranjiti akamshika mkono na kunaza kutembea naye kuelekea ndani.
“Hichi ndio chumba chetu tutakacho kaa hapa kwa miezi sita hadi mambo yatulie ndani ya Japani sawa mama”
Phidaya hakuzungumza kitu cha aina yoyote zaidi ya kutafuta sofa na kukaa, moyoni mwake akazidi kumchukia Ranjiti, hakumpenda kama asivyo mpenda Sheteni.
Taratibu dokta Ranjiti, akaanza kuvua nguo zake moja baada ya nyingine mbele ya Phidaya hadi akabakiwa na bukta ya ndani tu.
“Nimekumisi mke wangu”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akipanua mikono yake na kumkumbatia Phidaya aliye jikalia kwenye kochi, akimtazama kwa macho makali kuanzia juu hadi chini. Dokta Ranjiti, akaanza kunyonya shingo ya Phidaya, kuanzia upande wa kulie kwenda kushoto, juu kwenda chini.
Phidaya hakutikisika wala kuhisi kitu cha ania yoyote, mawazo yake yote yapo Japani kwa mwanaye Shamsa hakujua yupo kwenye hali gani kwa sasa. Hadi dokta Ranjiti anammalizia kumvua nguondipo Phidya akastuka, kutoka katika dibwi zito la mawazo.
“Unataka kufanya nini?”
“Phidaya alimuuliza kwa sauti ya ukali kiasi cha kumstua dokta Ranjiti aliye katika hisia kali za kimapenzi
“Ninahamu mke wangu”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa sauti ya mahaba, mazito
“Hembu niondolee upuuzi wako, nahitaji kwenda kuoga”
Phidaya alizungumza huku akitaka kunyanyuka kwenda bafuni, ila dokta Ranjiti akamzuia.
“Usitake nitumie nguvu”
Dokta Ranjiti alibadilika dakika hiyo hiyo na kuzungumza kwa sauti ya ukali, Phidaya hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali, mumewe kumfanya chochote ajisikiacho. Dokta Ranjiti akaanza kulifaidi tunda la Phidaya, kila alivyo zidi kufanya kitendo hicho ndivyo jinsi kumbukumbu za Phidaya zilivyo anza kumrejea kichwani mwake, akaanza kukumbuka jinsi mwanume wake wa zamani aliye jengeka kifua, alivyo kuwa akilala juu yake na kumkumbatia, mihemo yakimapenzi ya mwanaume huyo ilizidi kumfanya Phidaya kumbukumbu kurejea na kuiona sura ya mwanaume huyo, hakuiona sura ya dokta Ranjiti bali aliona sura ya mwanaume anaye kumbuka kwamba alimpenda sana kupita maelezo
“Mke wangu unanipenda…….”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akihema akijitajidi kukipandisha kiliama kirefu kwa kasi
“Ohooo yesssss nakupenda sana mume wangu EDDY”
Jina la Eddy likamfanya dokta Ranjiti, kasi, mashamsham yakupandisha mlima mrefu kukatika gafla, macho yakamtoka hakuamini kwamba kumbukumbu za Phidaya zimerejea.
***
Raisi mstaafu Praygod, baada ya kukabidhi nyaraka zote za serikali, kwa Mzee Godwion, hakuona haja ya kuendelea kukaaa nchini, kwa kutumia ndege yake binafsi aliyo kabidiwa na rafiki yake kipenzi Frennando ,yeye na mke wake, Rahab, wakiwa na walinzi wawili Pricsa na mllinzi wa kiume Emily wakaianza safari kwenda nchini Misri kwa ajili ya mapumziko kabla ya kwenda Mexco kuishi.
“Muheshimiwa kwa nini umeamua kuondoka mapema kiasi hichi nchini?”
Emily alimuuliza raisI mstafu bwana Praygod.
“Kwa sababu ya vitisho vya Godwin”
“Alikuambiaje?”
“Alinipa masaa ya kukaa nchini, sikuhitaji kulizungumza hilo mapema kwani lingezaa mtafaruku. Kwa sasa ninahitaji kuituliza akili yangu, nione kama miaka mingine mitano ijayo kama nitaweza kushinda uchaguzi”
“KKwa hiyo huto rudi tena Tanzania siku hizi za usoni?”
“Sijafikiria, au unashauri nini mke wangu?”
“Tuangalie upepo mume wangu”
Rahab alizungumza na kuendelea kucheza game kwenye simu yake, Priscar hakuzungumza chochote zaidi ya kuyasikiliza mazungumzo hayo.
“Ila ninawaonea sana huruma Watanzania, watanikumbuka”
“Kwa nini muheshimiwa?”
“Ahaa matokeo ya kura zao watayaona, tupo sisi tusikilizie itakuwaje”
Safari yao ilizidi kusonga mbele, wakiendelea kuzungumza wakijadili mstakabali wa nchi ya Tanzania unapo elekea, akazidi kuwafumbua masikio walinzi wake mambo ambayo yalifanywa na mzee Godwin akiwa jeshini hadi hapo alipo kuwa, kila mmoja akaonyesha wasiwasi wake juu ya hali itakavyo kutwa siku chache zijazo.
Wakafika nchini Misri majira ya saa nane usiku, balozi wa Tanzania nchini hapo akawapokea akiwa na ulinzi wa kutosha, moja kwa moja wakaelekea kwenye hoteli kubwa ya kifarahi, iliyo andaliwa kwa ajili yake apumzike hapo kwa kipindi chote atakacho yeye na mke wake pamoja na walinzi wao.
***
Mawazo mengi yakazidi kumuweka Eddy katika hali ya unyonge, hakutambua ni wapi alipo Phidaya. Siku zikazidi kuyoyoma, hapakuwa na matumaini yoyote ya kumuona Phidaya.
“Black Shadow”
Soroo alimuita Eddy mara baada ya kuingia kwenye pango hilo na kumkuta akifanya mazoezi ya viongo akiwa amevalia kinyago chake kichwani.
“Naam”
“Umesikia kwamba madam Phidaya ametekwa nyara?”
“Hapana kwani Phidaya ni nani?”
Eddy alijifanya hajui chochote ili azidi kupata habari kutoka kwa mtoto huyo aliye anza kumuamini sana kutokana na upeo wake wa akili kuwa mkubwa sana.
“Madam Phidaya ni mmoja wa wazamini wa kituo chetu, anatupatia misaada sana”
“Ahahaa anaonekana ana roho nzuri sana eheee?”
“Ndio ana roho nzuri. Pia ana mwanaye anaitwa Shamsa alikuja juzi juzi kuniangalia, ila alikuwa ana lia sana alipo kuwa akinitazama mimi”
“Kwa nini alikuwa analia?”
“Alisema kwamba nafanana sana na mdogo wake, anaitwa Junio”
Eddy kidogo, akakaa kimya, hakuzungumza chochote zaidi ya kumtazama Soroo kwenye mboni ya macho yake, kusema kweli Soroo anafanana na Junio kwa kiasi kikubwa, tofauti kati yao ni umri na kimo tu.
“Mbona umekaa kimya……”
“Hamna Soroo, rudi kituoni”
“Babu yupo wapi?”
“Amekwenda mjini”
“Sawa”
Soroo, akampa tano Black Shadow na kuondoka, machozi yakaanza kumbubujika Eddy usoni mwake, kila alipokuwa akimtazama Soroo akiondoka eneo hilo. Kumbukumbu za kifo cha Junio zikamjia kichwani mwake, akamkumbuka muuaji aliye husika na kifo cha mwaneye ni Manka. Eddy akatembea kwa hatua za haraka hadi kwenye moja ya droo akatoa kitabu chake kidogo cha kumbukumba alicho pewa na Mzee Yo, akaliandika jina la Manka kama mmoja wa watu wanao stahili kufa, huku juu ya jina hilo kukiwa na majina mawiliya ya mzee Godwin pamoja na dokta Ranjiti.
***
Akili ya dokta Ranjiti ikazidi kuchanganyikiwa, baada ya kugundua Phidaya kumbukumbu zake zinamrejea taratibu. Hakuwa na mbinu yoyote zaidi ya kuhakikisha anaimarisha ulinzi mkali kwenye eneo la chumba chake kuhakisha kwamba Phidaya hatoroki. Huduma zote za simu ndani ya chumba hicho akazikatisha, hakuhitaji Phidaya awasiliane na mtu wa aina yoyote.
Phidaya aliweza kulitambua hilo, kwamba mume wake haitaji akutane na mtu wa aina yoyote, maisha yake tangu afike Misri na kukaa ndani na kuangalia Tv pale dokta Ranjiti anapokuwa katika mizunguko yake ya kukutana na wafanya biashara wakubwa. Phidaya aliweza kuelewa njama za mume wake za kukataa yeye kuwa karibu na watu, akiamini kwamba ni lazima atawasiliana na watu ambao anawajua na itakuwa ni chanzo cha yeye kutorokla.
“Siwezi kuendelea kukaa humu ndani”
Phidaya alizungumza huku akivaa moja ya suruali aliyo nunuliwa na mume wake, akavalia na tisheti, kisha akasimama dirishani, hakuona haja ya kuvalia viatu kwani akili yake imemtuma kutoroka kupitia dirishani. Umbali wa gorofa kumi kwenda chini, haukumtisha alicho kikusudia ni kuhakikisha kwamba anatoroka ndani ya chumba hicho pasipo walinzi waliopo mlangoni kufahamu kitu kinacho endelea.
Akafungua vioo vya dirihani, achungulia chini, kashusha pumzi na kuanza kuutoa mguu wake wa kulia kwenye sehemu ulipo kanyaga mguu wake wa kulia, lengo lake alihitaji kwenda katika dirisha linalo fwata kwa kupita katika kijinjia hicho. Phidaya alipo hakikisha kwamba ameshikilia vizuri, akaanza kutambaa kuelekea kwenye dirisha la chumba cha pili, ila kabla hajafika akajikuta akigeuka na kuangalia chini, kizunguzuku kikali kikamshika na kujikuta akipepesuka, mikono na miguu yake vikapoteza muhimili na kujikuta akianza kuelea hewani na kwenda chini kwa kasi kali, kitendo kilicho shuhudiwa na watu wengi waliopo chini, kila mmoja alishangaa kuona mwanamke huyo akianguka kutokea gorofa ya kumi kuja chini.
SORRY MADAM (64)
Macho ya watu wengi yakashuhudia jinsi Phidaya anavyokuja kwa kasi chini, wakamshindikiza kwa macho yao hadi kwenye swimming poolm, lililo jaa maji liliopo chini usawa wa sehemu ambayo Phidaya aliangukia. Vijana wawili wenye asili ya kiarabu pamoja na Rahab ambaye alikuwa ameketi pembezoni mwa swimming pool hilo akipunga upepo wakajitosa kwenye maji, kila mmoja akiwa na lengo la kwenda kumuokuoa msichana huyo. Kwa pamoja wakajikuta wakimtoa kwenye maji, kidogo Rahab akaonekana kustushwa na msichana huyo. Kutokona ni mwanamke mwenzake Rahab akaanza kumpulizia hewa, Phidaya mdomoni mwake kumpa pumzi ya ziada kutokana kuanguka kwake kumemfanya kuzimia.
Haikuchukua muda Phidaya akastuka, huku akihema, macho yake yakatua kwa Rahab aliye muinamia, akashangaa kumuona Rahab kwa maana ni mtu anye mfahamu, ila bado hakujua ni sehemu gani ambayo aliweza kumuona mwanamke huyo.
Wahuduu wa Hoteli pamoja na meneja wa hotelo hiyo wakafika baada ya kujulishwa na wateja wao kwamba kuna tukio la ajabu limetokea, katika hoteli yao, wakakuta Phidaya akiwa amefunikwa na taulo, kubwa ili kutoa ubaridi mwilini mwake na mwili nzima unamtetemeka kwa woga.
“Yupo vizuri mpeni hewa musimzunguke”
Rahab alizungumza huku akiwasogeza watu waliopo katika eneo hilo, hapakuwa na mtu aliye weza kuamini kwamba mwanamke huyo anaweza kupona, hii ni kutokana na umbali mrefu alio weza kutoka hadi chini alipo angukia.
”Mama uaitwa nani?”
Meneje alimuuliza Phidaya, aliye mtazama kwa macho makali, yalio jaa wekundu ulio sababishwa na kulia sana.
“Kwa sasa hayupo sawa, labda badae anaweza kuzungumza”
“Kuna huduma ya dharura labda tuweze kumuwahisha hospitalini.”
“Hilo pia linaweza kusaidia”
Ikaletwa gari ya wagonjwa, Phidaya akaingizwa kwenye gari, huku Rahab akiomba na yeye kwenda, akakubaliwa, kutokana na msaada wake walio weza kuufanya kwa binti huyo. Haikuwachukua muda mwingi sana wakawa wamefika hospitalini, ila kabla Phidaya hajaingizwa katika chumba cha matibabu, akamuomba Rahab kuweza kuwasiliana na mtu aliye weza kumtajia namba yake.
“Huyo ni nani?”
“Ni mlinzi wangu”
“Yupo wapi?”
“Yupo Japani”
“Anaitwa nani?”
“Lee Si”
Phidaya alipo maliza kuzungumza hayo, kitanda alicho lalia kikasukumwa ndani ya chumba hicho kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa mwili wake.
***
“Lee Si nina mazungumzo na wewe”
Shamsa alizungumza huku akiufunga mlango wa Lee Si, baada ya kuugonga kwa muda kasha ukafunguliwa. Lee Si, akavaa tisheti yake kisha na kuelekea chumbani kwa Shamsa, akamkuta akiwa amekaa na Sa Yoo wakimsubiria, sura za wasichana hao zilimuonyesha Lee Si, kwamba wana maswali mengi juu yake.
“Nimefika”
Sa Yoo, akamkata jicho Lee Si kisha akamtazama Shamsa ambaye muda wote alikuwa akifikiria jambo la kuzungumza.
“Kwa nini unatuzunguka?”
Shamsa alizungumza huku akimtazama Lee Si usoni
”Kivipi madam?”
“Tuambie madam yupo wapi, ikiwa wewe kama mlinzi wake ni lazima utatambua kuna kitu kinacho endelea, la sivyo tutakuripoti polisi na utatuambia ukweli kuhusiana na sehemu alipo mama yangu”
Lee Si, akatabasamu kwa dharau kicha akamtazama Shamsa kuanzia chini hadi juu. Dharau ya Lee Si, ikamfanya Sa Yoo, kuachia msunyo mkali, huku akilitoa na yeye jicho lake kubwa fulani kumpandisha na kumshu Lee Si juu hadi chini.
“Hata mukinipeleka polisi, munahisi nitawekwa ndani? Siku ambayo mulikwenda kununuliwa nguo mimi nilikuwepo? Kama jibu ni hapana basi tambueni kwamba sifahamu alipo madam, na mimi nikama nyinyi sote hatujui ni wapi alipo”
“Shamsa unaona dharau zake nilizo kuambia, huyu ni lazima atakuwa anafahamu”
Sa Yoo, alizungumza huku akichukua mto mdogo wa kochi na kumrushia, Lee Si, na kumbamiza nao wa uso. Lee Si, akanyanyuka kwa hasira akamfwata Sa Yoo, sehemu alipo simama, kwa lengo la kumuadhibu kwa kitendo alicho kifanya ila kabla hajamfikia, akazuiliwa na Shamsa aliye simama kwa haraka.
“Unataka kufanya nini?”
Shamsa alimuuliza kwa sauti ya msisitizo huku akimtazama Lee Si usoni mwake, Lee Si akamsukumia Shamsa pembeni, akamzaba kibao kizito Sa Yoo, aliye baki akishangaa. Kitendo hicho kikamkera sana Shamsa, akanyanyuka na kumtandika kofi zito Lee Si, aliye mtolea macho makali Shamsa, akataka kurusha ngumi, ila simu yake, ikaita, akaitoa kwa haraka mfukoni mwa suruali yake, kabla hajatazama ni nani aliye piga simu hiyo, akastukia Sa Yoo, akimpiga teke kwenye mkono alio shika simu, ikaangukia pembeni.
Lee Si akamrukia Sa Yoo kwenye kochi kabla hajampiga kofi, tayari Shamsa Alisha jiachia, na kumrukia, akamuangusha chini na kuanza kumtandika ngumi mfululizo.
Lee Si hakukubali kuona anapigwa na msichana huyo alicho kifanya ni kujigeuza, akampiga Shamsa ngumi moja aliyo izuia kwa mikono yake miwili, Sa Yoo, katika kuzungusha zungusha jicho lake, akaiona simu ya Lee Si, ikiita, hakutaka kuujali ugomvi huo alicho fanya ni kuishika simu hiyo na kuipokea.
“Haloo”
Sa Yoo, alizungumza huku akikimbilia bafuni na kuwaacha Shamsa na Lee Si wakiendelea kupigana
“Unazungumza na Rahab Praygod ninatumaini kwamba wewe ndio Lee Si”
Sa Yoo, ikabidi kuitoa simu hiyo sikioni na kuitazama namba hiyo akagundua kwamba si namba ya Japan. Akili yake ikafanya kazi haraka haraka na kujibu kwamba yeye ndio Lee Si.
“Kuna taarifa ambayo bosi wako Phidaya ameniambia nikujulishe, kwa sasa yeye yupo nchini Misri barani Afrika na yupo hospitalini kwa uchunguzi zaidi wa madaktari hii, ni baada ya kujaribu kufanya jaribio la kutaka kujiua”
Sa Yoo, akauziba mdomo wake kwa wasiwasi mwingi, akionekana kustushwa na habari hiyo.
“Alooo unanisikia?”
Rahaba alizungumza baada ya kuona mtu anaye zungumza naye amekaa kimya.
“Nakusikia, amelazwa hospitali gani?”
Rahab akalitaja jina la hospiali aliyo lazwa Phidaya, kisha akamuaga Lee Si, kutokana na kumaliza mazungumzo yake aliyo kuwa ameagizwa na Phidaya. Sa Yoo, akatoka bafuni na kurudi sebleni, akamkuta Lee Si, akiwa anavuja damu puani huku amelala sakafuni na Shamsa amesimama pembeni yake huku amekunja ngumi na kufura kwa hasira.
“Vipi?”
Sa Yoo, alimuliza Shamsa huku akiwa amemkodolea macho Lee Si, anaye jizoa zoa kunyanyuka.
“Siwezi pigana na wazembe mimi”
Shamsa alizunguza huku akiondoka karibu na Lee Si, aliye kaa kitako sakafuni akiwa haamini kwamba umahiri wake wa kupigana ameweza kuchezea kichapo ambacho hakukitarajia kabisa kutoka kwa binti huyo ambaye kwa mara ya kwanza alimchukulia binti wa kawaida.
“Nenda chumbani kwako na usije ukarudia”
Kwa haraka Sa Yoo akaituma kwa namba ya simu kwa ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu yake, namba ambayo ilipiga kwenye simu ya Lee Si, kisha akaifuta na kumrushia Lee Si simu yake.
“Besti hiyo puaa ilivyo kaa”
Sa Yoo alimtania Lee Si baada ya kumuona pua yake ikiwa kidogo kama imepinda, huku damu zikiendelea kumwagika. Baada ya Lee Si kutoka chumbani hapo, na Sa Yoo kuhakikisha kwa kuchungulia mlangoni kwamba Lee Si ameingia chumbani kwake akamuelezea Shamsa kila kitu alicho kizungumza kupitia simu ya Lee Si.
“Huyo mtu amesema kwamba anaitwa nani?”
“Rahab Praygod”
Jina la Rahab Praygod halikuwa ngeni masikioni mwake, ila hakuhitaji, kuliwekea maanani kwa maana majina duniani yananafanana isitoshe kwamba mtu mwenyewe aliye ipiga simu hiyo yupo nchini Misri.
“Inabidi tuondoke”
“Sawa tuanze kufwatilia maswala ya viza”
“Poa”
***
Macho ya Sabogo yaliweza kuwakumbuka Shamsa na Sa Yoo, ambao amewaona wakiwa wamesimama kwenye ofisi za shirika moja la ndege. Kutokana alisha elezwa na Black Shadow kuhusiana na binti huyo kwamba ni mwanae hakuona haja ya kuendelea kuwatazama. Akatembea kwa mwendo wa haraka hadi walipo, akamgusa Shamsa begani na kufanya Shamsa kugeuka na Sa Yoo pia kugeuka. Wote wakaonekana kumshangaa, Sabogo kwani ni jitu refu kwenda juu, na wote vimo vyao wanamfikia kiunoni.
“Ninaweza kuzungumza na nyinyi?”
Sa Yo alikubali kwa kutingisha kichwa kutokana na woga ulio mvaa gafla. Wakatoka hapo dirishani na kwenda kukaa nje ya uwanja huo wa ndege ambapo kuna mgahawa
“Naamini kwamba munanifahamu?”
“Hapana”
Sa Yoo alijibu kwa haraka sana hata kabla Shamsa kujibu.
“Mimi ni meneja wa Black Shadow ninaimani kwamba wote munamjua, ninaitwa Sabogo”
“Ahaaa wewe ndio yule ambaye ulituletea tiketi za kukaa VIP?”
“Ndio mimi haujakosea”
Furaha ikamuingia Shamsa, akaona ni bahati kubwa sana kuonana na mtu huyo kwa maana ndoto za kukutana na mpenzi wake ambaye ni Black Shadow, zinaanza kufufuka upya.
“Black Shadow yupo wapi?”
“Yupo na ninaimani pia atakuwa na furaha kuonana na nyinyi”
“Ninakuomba utupeleke sasa hivi”
Shamsa alizungumza huku akimshika, mkono Sabogo.
“Kwa mchana huu ninaimani itakuwa ni ngumu labda kwa usiku”
“Hata iwe saa nane ya usiku mimi nipo tayari kuonana naye”
“Sawa kuna sehemu nitawahitaji muje, ila hakikisheni kwamba munakuja nyinyi wawili peke yenu tu”
“Sawa”
Sabogo akaawachia namba za simu, hata wazo la kwenda Misri, barani Afrika, wakaliweka kando kwanza, moyo wa upendo juu ya Black Shadow, ukarudi kwa upya kabisa moyoni mwa Shamsa. Siku hiyo furaha ikamjaa tele moyoni mwake, hata kumbukumbu alizo ambiwa na Phidaya kwamba Black Shadow ni baba yake ziliteketea. Hakutaka kuzipa uzito wa aina yoyote kutokana anaamini kwamba Black Shadow ni mwanaume mwengine kabisa na Eddy ni mwanaume mwengine kabisa.
***
Furaha na amani ikamtoweka Madam Mery, hakujua maisha yake ya hapo mbeleni yatakuwa vipi, kwani adui yake namba moja ndio huyo amekalia kiti cha uraisi nchini Tanzania.
“Nitafanyeje?”
Ndio swali ambalo Madam Mery aliendelea kujiuliza kichwani mwake, akaendelea kuzunguka chumbani kwake, akitafakari, hakuhitaji siku hiyo kuonana na mtu wa aina yoyote hata wafanyakazi wake wa ndani. Kila alilo lifikiria alilipangua, kwani mpango wake aliona unafeli.
“Eddy, lazima nionane na Eddy ndio mtu pekee ambaye anaweza kuniunga mkono katika mpango wangu huu”
Madam Mery alizungumza huku akiifungua Laptop yake, akaanza kutafuta ni wapi alipo Eddy. Ripoti ya mwisho ambayo aliipata katika mtandao kwamba Eddy yupo Japani na nimuhalifu katika nchi hiyo anatafutwa.
Madam Mery hakuona haja ya kupoteza muda akakata tiketi kabisa kupitia mtandao, siku iliyo fwata akapanda ndege hadi Dar es Salaam, ambapo akakuta tiketi yake ikiwa tayari, akapanda ndege ya shirika la KLM na kuianza safari yake, ambayo ilimchukua masaa mengi kukaa angani.
Kitendo cha kutoka katika uwanja wa ndege akamshuhudia Shamsa akiwa na binti mmoja wakiingia kwenye gari ya kifahari na kuondoka.
Madam Mery hakuhitaji kuweka hisia za kwamba mtu aliye weza kumuona ni tofauti za Shamsa, kutokana binti huyo anamtambua vizuri sana na Alisha wahi kukaa naye na kumueleza siri nyingi kuhusiana na kikosi cha siri kinacho milikiwa na mzee Godwin baba yeka Eddy.
Madam Mery akamuomba dereva huyo kulifwata gari hilo kwa nyuma popote litakapo kwenda, dereva naye akafanya hivyo kama alivyo agizwa, gari hilo likafika kwenye moja ya hoteli mabinti hao wakashuka, Madam Mery naye akashuka na kumlipa dereva pesa yake akiamini kwamba atawakuta mapokezi Shamsa na huyo rafiki yake wa kijapani.
Hadi anaingia ndani hakuweza kuwaona, muhudumu mmoja akamkaribisha, bila kutaja haja yake, ya yeye kumfikisha hapo, ikamlazimu kuchukua chumba katika hoteli hiyo hiyo, akijipa moyo kwamba akiliona gari hilo basi Shamsa atakuwa amemuona na kama amemuona Shamsa basi Eddy hato kuwa mbali na atamueleza kila kitu kuhusiana na Tanzanani.
***
Sabogo, mara baada ya kurudi katika makao yake, kitu cha kwanza alicho kifanya akampigia simu Black Shadow na kumuomba aweze kukutana naye kwenye moja ya gorofa juu kabisa ya gorofa hilo zinazo pata gorofa, ishirini na tano.
“Kuna nini?”
“Kuna zawadi nimekuandalia”
“Sawa kaka”
Majira ya saa nne usiku, Sabogo akawa ndio mtu wa kwanza kuweza kufika katika eneo la gorofa hilo, akawaelekeza Shamsa na Sa Yoo, mara baada ya kupigiwa simu na wasichana hao. Haikuchukua muda sana Sa Yoon a Shamsa wakawa wamesha fika katika kilele cha gorofa hilo.
“Yupo wapi Black Shadow?”
Shamsa alimuliza Sabogo.
“Ninaimani kwamba yupo njiani”
Ikawalazimu wawe wavumilivu waendelee kumsubiria Black Shadow.
***
Katika kitu ambacho kilitoke kumkera na kumuudhi Lee Si ni kupigwa na Shamsa, bado hakuwa anaamini kwamba amechezea kichapo kikali kutoka kwa binti huyo. Moyoni mwake akajiapiza kuweza kumuua, iwe isiwe ni lazima awaangamize hususania cha umbea Sa Yoo.
Akiwa chumbani kwake majira ya usiku, aliweza kuusikia mlango wa Kina Shamsa ukiwa unafungwa kwa nje, akatulia kidogo na kuweza kutoka kuchungulia kuona ni wapi wasichana hao wanapo elekea, akawaona wakondoka aneo hilo wakiwa wamevalia vizuri.
“Hii ndio nafasi yangu”
Lee Si alizungumza huku akirudi ndani, akachukua bastola zake mbili, akiamini kwamba Shamsa na Sa Yoo, wanakwenda disko kuburudika baada ya siku yao kuwa mbaya. Akavaa koti lake jeusi pamoja na gloves nyeusi mikononi mwamke.
Akashuka kupitia lifti hadi chini kabisa na kuwashuhudia Shasma na Sa Yoo wakiingia kwenye gari ambalo ni mali ya Phidaya. Wakaondoka eneo la hoteli kwa haraka na yeye akakimbilia hadi sehemu ya maegesho alipo liacha gari lake. Akaingia na kuanza kulifwatilia Shamasa na Sa Yoo kwa umakini mkubwa pasipo wao wenyewe kuweza kustukia. Akawashuhudia wakiingia kwenye moja ya mtaa mbao unasifika kwa vibaka na uporaji wa mali za raia wema.
Akawashuhudia wakisimamisha gari lao kwenye moja ya gorofa, wakaingia kwenye gorofa hilo, kwa haraka na yeye akashuka kwenye gari na kuanza kupandisha kwenye gorofa hilo. Akaendelea kuwafwata kwa umakini wa hali ya juu hadi gorofa ya mwisho, akawaona wakiendelea kupanda juu ambapo ni juu kabisa.
“Wanakwenda wapi hawa?”
Lee Si, alijiuliza kwani woga ulisha anza kumuingia na kuhisi kwamba huwenda anavyutwa kwenda juu zaidi akihisi kwamba amesha stukiwa. Pua yake aliyo ifunga plasta kubwa nyeupe kutokana na kipigo kikali, ikaanza kumuuma. Kutokana na hewa nzito aliyomo katika chumba alicho jificha, kwani gorofa hiyo halitumiki, na lipo katika harakati za kuvunjwa na serikali na kujengwa upya kwani ni moja ya gorofa la zamani ndani ya Japan katika mji wa Yokohama.
Lee Si akachungulia nje, akamshuhudia mtu anaye mtafuta siku zote, Black Shadow, akimalizia kupandisha ngazi kwenda juu walipo elekea Shamsa na Sa Yoo.
“Bingooo”
Lee Si alizungumza huku akiwa amejawa na furaha moyoni mwake, akachomoa bastola yake moja, akaikagua inarisasi za kutosha, akakuta magazine ya bastola hiyo ikiwa na risasi za kutosha. Akaanza kupandisha kwenda juu kabisa, huku akinyata. Akakuta mlango wa kufikia juu kabisa ukiwa wazi kidogo. Akausukuma taratibu, akachungulia, akamuona Black Shadow akiwa amekumbatiana na Shamsa aliye jawa na tabasamu usoni mwake hadi machozi yakimwagika. Pembeni yake alimuona Sa Yoo naaye akiwa na furaha, huku jitu kubwa ambalo hakuwahi kuliona siku hata moja, nalo likiwa limeshika kitambaa mkononi mwake na kujifuta machozi.
Lee Si, akainyanyua bastola yake mbele taratibu, akainyoshea walipo maaduia zake, akawatazama wote haraka haraka, kisha akaftyatua risasi moja. Mlio wa bastola ukawastua wote, kila mmoja mmoja alimtazama mwenzake kuona risasi hiyo imempiga nani, kisha wote macho yao wakayatupia sehemu ilipo tokea risasi hiyo, wakamuona Lee Si akiwa ameshika bastola, akihitaji kufyatua risasi ntingine kwao.
==>ITAENDELEA...
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com
Post your Comment