Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » Jux apewa heshima kubwa Burundi, asema haijawahi kutokea kwa msanii yeyote

Jux apewa heshima kubwa Burundi, asema haijawahi kutokea kwa msanii yeyote

Written By Bigie on Monday, February 19, 2018 | 12:23:00 PM

Mkali wa muziki wa RnB Bongo, Jux amepewa love ya kutosha weekend iliyomalizika wakati alipokuwa akifanya show nchini Burundi.

Muimbaji huyo wa ngoma ‘Utaniua’ amesema licha ya mvua kunyesha bado watu walijitokeza kwa wingi kushuhudia burudani kutoka kwake.
 
Katika moja ya video alizoweka Jux katika social network zake anaoneka akivalishwa ‘vitu’ vya asili mkono pamoja na kichwani kama ishara ya heshima na kutambua uwepo wake nchini humo.
 
“We made a history nashukuru kwa heshima yenu ya kuniimbia wimbo wa taifa kama heshima yenu kwangu na hii haijawahi kutokea kwa Msanii yoyote yani yote aliyeshawahi kuja burundi Asanteni sana sana,” amesema Jux.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya