Lile bifu kiboko lililokuwa likiendelea kati ya Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan (CCM) na Shyrose Bhanji aliyechanguliwa kuwa mbunge Afrika Mashariki hivi karibuni limekwisha
Bifu hilo ambalo lilitokana na mchakato wa kuwania ubunge wa Kinondoni wakati wa kura za maoni katika uchaguzi mkuu mwaka 2010, sasa limeyuka rasmi baada ya waheshimiwa hao kuthibitika kuwa wanapata muda wa ‘kuchati’ na kusalimiana huku Shyrose akikubali yaishe hasa walipokutana kwenye mchakato wa kugombea nafasi ya ubunge wa Afrika Mashariki.
Ilielezwa kuwa hata fomu za kugombea ubunge wa Afrika Mashariki zilikuwa chini ya Azzan hivyo Shyrose hakupata tabu kuzipata.
Mbali na hilo, ilifahamika kuwa Azzan alimtoa woga Shyrose na kumpigia debe, jambo ambalo mwanadada huyo hakuliamini hadi alipopata nafasi hiyo.
Akizungumzia ishu hiyo, Azzan alikiri kumaliza mgogoro huo kwa kumpigia debe hasimu wake huyo hadi akachukua nafasi ya ubunge wa Afrika Mashariki.
Post your Comment


