Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, marehemu Patrick alipata ajali maeneno ya TAZARA alipokuwa akiendesha gari na kujaribu kumkwepa mwendesha pikipiki na kwa bahati mbaya gari lake likakosa uelekeo na kuingia mtaroni na kusababisha ajali iliyomwacha na majeraha makubwa ambapo aliaga dunia muda mfupi baadaye.
Patrick alijiunga kuichezea Simba SC akitokea timu ya Azam FC. Video za baadhi ya magoli aliyowahi kufunga zipo youtube.
Patrick alizaliwa tarehe 9 Machi 1980 mjini Kinshasa, Kongo D.R.C.
Alikuwa raia wa Rwanda.Amefariki siku chache tu baada ya kocha wa timu ta taifa ya Rwanda kumuita kujumuika katika timu ya Taifa ya nchi hiyo.
Poleni nyote mliofikwa na huzuni ya msiba huu!
Apumzike pema Patrick Mafisango.
AMIN.
Post your Comment