
Kutoka kushoto ni Afisa wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani, Agnes Lusinde, Loveness Mamuya , Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Iddi Sandaly na Jacob Kinyemi wakiwa nje ya Hotel katikati ya Jiji la Washington, DC wakisubili kusalimiana na Mhe. Rais Dkt. Jakaya Kikwete ambae yupo Nchini Marekani kwa mwaliko wa Rais Barack Obama ambayo pamoja na mambo mengine, atashiriki mkutano wa Nchi Nane Tajiri Duniani (G8) utakaofanyika Camp David na kuhutubia mkutano wa dunia kuhusu usalama wa chakula.
Rais Kikwete ni miongoni mwa marais wanne wa Afrika walioalikwa kwa ajili ya mkutano huo. Wengine ni Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Yayi Boni wa Benin, Rais John Mills wa Ghana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi.

Viongozi wa Jumuiya na Watanzania wengine waliogombea nafasi za uongozi, DMV wakijumuika pamoja na baadhi ya Wajumbe waliokuja na msafara wa Mhe. Rais kwa vitafunio na vinywaji laini Hotelini hapo.

Juu na chini ni Viongozi wa Jumuiya na Watanzania waliogombea nafasi mbali mbali za uongozi DMV wakiwa na mmoja wa kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania New York, Shabani Mseba (kulia) waipata picha ya pamoja


Mhe. Rais akiingia ukumbini huku akilakiwa na Mhe. Christopher Chiza, Waziri wa Kilimo, Chakula na Lishe

Mhe. Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Kaimu Balozi Mhe. Lilian Munanka, kushoto kwa Mama Munanka ni Afisa Ubalozi Abbas Missana, Afisa Suleiman Saleh na Afisa Agnes Lusinde.

Mhe. Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Afisa Ubalozi Suleiman Saleh

Mhe. Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Afisa Ubalozi Asia Dachi

Aliyesimama ni Loveness Mamuya mmoja wa wagombea uongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV, akijitambulisha kwa Mhe. Rais, Dkt Jakaya Kikwete.

Aliyesimama ni Aziz nae akijitambulisha kwa Mhe. Rais Jakaya kikwete

Aliyesimama ni Shaban Mseba, kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania, New York nae akijitambulisha kwa Mhe. Rais Jakaya Kikwete.

Aliyesimama ni muweka Hazina wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Ndugu Genes Malasy akijitambulisha kwa Mhe. Rais Jakaya Kikwete.

Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Ndugu Iddi Sandaly akijitambulisha kwa Mhe. Rais Iddi Sandaly.




Post your Comment