Ni wakati wako kijana,
Historia inaonyesha wazi kuwa hakuna mwanasiasa mashuhuri hapa duniani aliyeanzia siasa akiwa mzee, chimbuko la mwanasiasa bora lazima lianzie kwenye harakati za ujana hasa ikizingatiwa kuwa moja ya sifa za mwanasiasa bora lazima awe jasiri.
Awe mtu aliyejitoa kwa dhati kupinga vitendo vyote dhalimu,awe mzalendo anayeipenda na kuitetea nchi yake wakati wowote, awe kiongozi anayechukia ufisadi, rushwa, uongo, uchochezi na aina yoyote iwayo asiwe mbaguzi na mwenye kuunda
makundi ya chuki na fitina.
Hapo ndipo chimbuko la mwanasiasa bora linapoanzia na kikubwa zaidi lazima mtu wa aina hiyo awe na uchungu mkubwa dhidi ya binadamu wenzake wanaopenda kukiuka haki za binadamu wenzao kwa ajili ya manufaa yao binafsi na wale wanaopenda kujilimbikizia mali huku wengine wakifa kwa shida.
Mwanzo na dalili za kumuona mwanasiasa bora ndipo zinapoweza kuchambuliwa na sifa hizo na nyingine nyingi ndizo zilizowazalisha wanasiasa na wanaharakati wengi wa haki za binadamu ambao kwa ushawishi wao wamefanikisha mapinduzi ya kiuchumi ndani ya nchi zao.
Wale walioamua kujiingiza kwenye siasa kwa lengo la kutafuta utajiri ndio hao hao waliochangia kuifikisha nchi hii hapa ilipo na hawana sababu zozote za kusifia mafanikio wanayoyataja leo kuwa yametokana na uongozi wao uliotukuka kumbe kazi
waliyoifanya ndio hii inayoibua kwa kasi wanasiasa vijana.
Ukweli utabaki pale pale kuwa, Rais wa awamu ya kwanza wa nchi hii, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alianza siasa akiwa kijana mbichi, alibebwa na sifa zote nilizozitaja hapo juu, alikuwa jasiri, aliipenda nchi yake na watu wake na hakuwa hata
na chembe ya ubaguzi.
Kwa kuwa dhamira ya kweli ilimuongoza katika ukweli,uadilifu na kujitoa zaidi kwa ajili ya kupigania haki za wanyonge hakuona shida kupoteza kazi yake ya ualimu ili aingie kwenye siasa, alibaki kuwa mwalimu bora na atakumbukwa daima kama mwalimu.
Post your Comment


