Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » HUKUMU YA KESI YA JOHN MNYIKA NI MEI 24 2012

HUKUMU YA KESI YA JOHN MNYIKA NI MEI 24 2012

Written By mpekuaji on Saturday, May 5, 2012 | 10:09:00 AM


Mbunge wa Ubungo, John Mnykka (CHADEMA) anatupasha katika blogu yake  haya yafuatayo:

Tumemaliza majumuisho ya kesi dhidi yetu. Hukumu imepangwa kutolewa tarehe 24 Mei 2012. Mawakili wote wawili wa upande wa utetezi wametimiza wajibu wao.

Pamoja na kuwa mawakili kwa ujumla walizungumza kwa zaidi ya saa saba, namnukuu kiduchu Wakili wetu Mbogoro: “Mshindi wa uchaguzi anatokana na maamuzi ya watu wengi, haki ambayo huipata kwa nadra kila baada ya miaka mitano na ni mchakato unaotumia fedha nyingi za walipa kodi. 

Hivyo kiwango cha uthibitisho wa madai yoyote lazima kiwe bila ya shaka yoyote... mlalamikaji Hawa Ng’umbi amesema mwenyewe mahakamani kuwa hana tatizo na matokeo ya toka vituoni, malalamiko yake sio juu ya nani mshindi. 

Kwa kawaida kesi za uchaguzi hufunguliwa na wenye kupinga ushindi wanaodai kuwa wangeshinda wao iwapo sheria zisingekiukwa; kama hapingi matokeo ya vituoni ambayo majumuisho yake ndio yamempa Mnyika ushindi; tunaweza kujiuliza tuko hapa kwa ajili gani?” 

Tuungane pamoja katika sala na swala kumwombea kwa Mwenyezi Mungu Jaji Upendo Msuya afanye maamuzi ya haki.

JOHN MNYIKA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts