Baada ya hayo, pia Usher Raymond nae aliieleza mahakama jinsi mkewe wa zamani alivyo na mfululizo wa matukio mabaya huku akielezea pia wasiwasi juu ya watoto wake kama wanapata matunzo sahihi kutoka kwa mama yao.
Amesema Tameka ambae ana zaidi ya umri wa miaka 40 amewahi kutaka kupigana wakati Usher alipokwenda nyumbani kwa Tameka akiwa ameambatana na mpenzi wake mpya (Grace Miguel) ambae pia ni meneja wake.
Walipokua mahakamani, Usher Raymond pia alikanusha tuhuma kwamba alikua akitumia vilevi mbele ya watoto wao wawili wa kiume, Usher na Tameka ambao walioana mwaka 2007 na kuachana kabla ya kufikisha miaka miwili.
bado wako mahakamani na ishu kubwa bado ni watoto.
Post your Comment


