Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » MBUNGE WA ARUMERU MASHARI,MH NASSARI ATAKA VIJANA WAACHE KUNYWA VIROBA

MBUNGE WA ARUMERU MASHARI,MH NASSARI ATAKA VIJANA WAACHE KUNYWA VIROBA

Written By mpekuaji on Tuesday, May 15, 2012 | 9:02:00 AM


MBUNGE wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema), amewasihi vijana, kujifunza uwajibikaji na kuachana na starehe zisizo za msingi hususani unywaji wa pombe ya kupindukia aina ya “viroba”.

Nassari alisema unywaji huo wa pombe kupindukia, hautawasaidia kwa sasa katika karne hii, bali kwani vijana wanapaswa kuwa na maono yenye tija katika kujiletea maendeleo wenyewe na kuondoa dhana tegemezi.

Nassari aliyasema jana katika hafla ya uzinduzi wa kituo cha watoto yatima cha African Orphanage kilichopo Sakila, ambao ulienda sanjari na sherehe za kumuaga mwinjilisti mkuu na mwasisi wa makanisa ya Pentekoste wilayani Arumeru, Askofu Nickson Issangya anayeenda kuhubiri Injili nje ya nchi Afrika na barani Ulaya.

Aidha, alisisitiza kwa wananchi katika jimbo hilo kushikamana kwa pamoja na kusahau itikadi zao za kisiasa kwani muda wa kampeni umemalizika na mbunge amepatikana.

Alisema wakazi wa jimbo hilo wengi wao wamekuwa wakijengeana chuki zinazosababishwa na tofauti za kisiasa hadi makanisani bila kutambua kuwa uchaguzi sasa umemalizika na kinachotakiwa ni kuwajibika kwa kufanya kazi za kuleta maendeleo katika jimbo hilo na taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine, mbunge huyo alitoa ushuhuda wa maisha yake na kudai kuwa wakati akisoma shule ya msingi, alikuwa akiuza kwa kutembeza minadani mifuko aina ya plastiki maarufu kwa jina la Marlboro, kwani wazazi wake hawakuwa na uwezo wa kumlipia ada.

Alisema wakati akisoma alipandikizwa maono ya ubunge na Mwenyezi Mungu, hivyo katika kipindi chote cha masomo yake kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu, ndoto zilizokuwa zikimjia usingizini ni kuhusu kuwa mbunge.

Aliwataka wananchi katika jimbo hilo kushikana katika kuliletea maendeleo jimbo hilo, lenye changamoto nyingi ikiwamo ya uhaba wa ardhi na kudai kuwa atafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha analeta mabadiliko na kwamba hawatajuta kumchagua.

Kwa upande wake, Askofu Issangya aliwaomba wakazi wa jimboni humo kuacha kubaguana kwa itikadi za kisiasa hadi makanisani na kuwataka kupigania maendeleo yao wenyewe wakimtumaini Mwenyezi Mungu kwa kuwa kampeni za uchaguzi zimemalizika na mbunge amepatikana.

Katika sherehe hiyo, Nassari aliahidi kusaidia vituo vyote vya watoto yatima vilivyomo katika jimbo hilo na kuwataka wananchi kujikita zaidi kutoa msaada kwenye makundi yasiyojiweza hususani yatima, wajane na kinamama wazee, kwani kabla ya kuwa Mbunge, alikuwa na kituo cha yatima 86 aliokuwa akiwahudumia.

Chanzo: Habarileo

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts