Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » UWOYA ADAIWA KUMUUA MWANAYE

UWOYA ADAIWA KUMUUA MWANAYE

Written By mpekuaji on Monday, May 7, 2012 | 10:37:00 AM

JAMBO limezua jambo! Ujauzito anaodaiwa kubebeshwa Irene Pancras Uwoya, umezua kizaazaa Habari zilizozagaa kwenye ulimwengu wa mastaa wa Kibongo zinatonya kuwa, mwanaume anayedaiwa ‘kumshibisha’ Uwoya aliyetajwa kwa jina moja la Ababuu ambaye ni mwenyeji wa Kilimani visiwani ZanziIrene Pancras Uwoya (pichani anavyoonekana kwa sasa) ambaye hivi karibuni aligandwa na skendo ya kubeba ujauzito nje ya ndoa, anadaiwa ‘kuua’ kichanga kilichokuwa tumboni mwake.

Hayo yameibuka baada ya juzikati Uwoya ambaye ni mke wa msakata kabumbu wa Timu ya Rayon Sports FC ya Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ kuonekana hana mimba huku madai yakiwa ni kwamba kitumbo kimeyeyuka ghafla.

Rafiki yake atoboa

Kwa mujibu wa mmoja wa marafiki wa karibu wa staa huyo, alishangazwa alipomuona Uwoya akiwa tofauti na alivyomzoea (mwenye kitumbo) huku taarifa zikienea kwa kasi kuwa amechoropoa.

“Alikuwa nayo tena ilifikia miezi minne na haikuwa siri, lakini cha ajabu nimemuona hana, inavyoonekana atakuwa ametoa baada ya kuhisi itamtibulia ndoa yake,” kilidai.
Uwoya anasemaje?

Ili kupata mzani wa habari hiyo, mwandishi wetu alimtafuta Uwoya kuzungumzia madai hayo ya kupoteza kichanga kilichokuwa tumboni mwake ambapo alikana kufanya ukatili huo na kudai kuwa ni uzushi.

“Haa! Hiyo kitu hakuna na laiti ningekuwa na huo ujauzito unaofanyiwa matangazo, nisingeutoa kwani nimezaliwa na nahitaji kuzaa, hao wanaonitangazia hizo habari waambie wakupe uthibitisho,” alisema Uwoya.
tujikumbushe

Miezi kadhaa iliyopita Uwoya alidaiwa kuwa na ujauzito ambapo mwanaume aitwaye Ababuu alitajwa kuwa mhusika huku msanii huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja (Krish) akikwepa kulizungumzia hilo lakini akakaririwa na jarida moja litokalo mara moja kwa mwezi la Machi akikiri kuwa mjamzito.

CHANZO: IJUMAA WIKIENDA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts