Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » Valérie Trierweiler: FIRST LADY ASIYE NA PETE YA NDOA KIDOLENI

Valérie Trierweiler: FIRST LADY ASIYE NA PETE YA NDOA KIDOLENI

Written By mpekuaji on Monday, May 14, 2012 | 7:58:00 PM


Wimbi la mabadiliko katika nyanja za kisiasa duniani hivi karibuni lilitua nchini Ufaransa.Wananchi wa nchi hiyo inayosifika sana kwa kuwa na wanawake ambao siku zote wana uzito wa kati na wanaopenda sana masuala ya mitindo na urembo,wakaamua kumuondoa madarakani Bwana Nicholaus Sarkozy (President Bling Bling) na kumuingiza mjamaa François Hollande.

Baada ya uchaguzi huwa macho na masikio yanaelekezwa kwingine.Ni kawaida katika siasa.Hapo ndipo linapokuja suala la First Lady.Kama utakumbuka,Sarkozy aligonga vichwa vya habari ulimwenguni mwaka 2008 alipoamua kufunga ndoa na Carla Bruni baada ya kutalakiana na mkewe wa pili. Hiyo ikawa ni ndoa ya tatu kwa Sarkozy. Akamuoa Carla Bruni,mrembo wa kusifika ambaye pia ni mwanamuziki.Sarkozy akaendeleza sifa ya kuonekana mtu wa totoz.

Sasa kama Wafaransa walidhani masuala ya “chumbani” ya Ikulu yangeishia kwa Sarkozy, pengine hivi sasa wanagundua kwamba sio kweli. Hollande naye yumo na ana yake. Wakati kampeni za uchaguzi zilipopamba moto, Hollande alionekana wazi kuwa na mwenzake. Wanaohoji wakaanza.Nani yule? Wakaambiwa well…ni girlfriend. Hapana ni mkewe.Ahh wapi.

Baadaye ikawa wazi kwamba wawili hao sio mke na mume.Wote walishaonja ndoa wakatalakiana na wenzao.Hivi sasa wapo pamoja na wanaingia Ikulu kuweka historia mpya!

Kwa mara ya  kwanza katika historia ya Ufaransa kuwa na Rais na First Lady wanaoishi pamoja katika Ikulu ya nchi hiyo (Élysée Palace) ambao kimsingi  na kisheria sio mke na mume. Valérie Trierweiler na François Hollande hawajaona. Katika kiingereza wanatambulishwa kama Partners.

Valérie Trierweiler mwenye umri wa miaka 47 ni mwandishi wa habari na mtangazaji mzoefu wa televisheni. Ameshawahi kutalakiwa mara tatu na ana watoto watatu.

Lakini wakati mazungumzo haya ya kuwa na First Lady asiye na pete ya ndoa kidoleni yakiendelea,kuna uvumi kwamba huenda Valérie Trierweiler na François Hollande wakaoana wiki hii.Huenda wakaona hata kabla ya safari yao ya pamoja ya kimataifa katika mkutano wa G8 unaotarajiwa kufanyikia pale Camp David katika viunga vya Maryland nchini Marekani kuanzia tarehe 18-19 Mei.

Hayo ndiyo yanayojiri nchini Ufaransa!

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts