Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » WATANGAZAJI WA KIKE WAUNDA KUNDI LA KUSAIDIA WANAWAKE WASIOJIWEZA

WATANGAZAJI WA KIKE WAUNDA KUNDI LA KUSAIDIA WANAWAKE WASIOJIWEZA

Written By mpekuaji on Thursday, May 24, 2012 | 9:59:00 AM


Gea Habib.


Watangazaji wa kike kutoka vituo mbalimbali vya runinga na redio nchini, wameunda kundi litakalojulikana kama Umoja wa Watanzangaji Marafiki Tanzania ambalo litakuwa na kazi ya kuwasaidia wanawake wasiojiweza.

Habari zilizovuja kutoka miongoni mwa wanaounda kundi hilo zilisema kuwa, kundi hilo litaundwa na wanaharakati kama Maimartha Jesse, Sauda Mwilima, Zamaradi Mketema, Dina Marios, Gea Habib na wengine wengi.


Mpenyesha habari huyo aliendelea kusema kuwa, kundi hilo litakuwa na jukumu la kutoa mitaji kwa vikundi vya wanawake wasiojiweza na kutoa elimu ya ujasiriamali.


Baada ya kuzidaka habari hizo, Mwandishi wetu alifanya juhudi za kumsaka mmoja wa wanaodaiwa kuunda kundi hilo, Maimartha ambaye alikiri kuundwa kwa kundi hilo na wanaharakati hao na kudai kuwa bado mapema kulizungumzia kwa undani zaidi.


“Ni kweli kundi hilo lipo lakini bado mapema sana kulizungumzia kwani kuna mambo bado tunakamilisha ndipo tutaweka kila kitu hadharani,” alisema Maimartha.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts