Home »
JAMII
» Watuhumiwa Wa Vurugu Za Mkutano Wa Chadema Nduli Wafikishwa Mahakamani
 |
Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakifika Kituo cha Polisi Iringa. |
 |
|
Washtakiwa wa kosa la kujeruhi Ndugu Meshaki Chonanga, Alex Chonanga, Greyson Chonanga na Musa Mtete wote kwa pamoja wakitoka Mahakamani leo baada ya kusomewa shitaka la kuwajeruhi Ndugu Suleiman Komba, Peter Mselu na Oscar Sanga. Washtakiwa walikana kosa hilo na kesi yao kuahirishwa mpaka tarehe 25/05/2012 |
|
 |
Washtakiwa wakishuka kwenye Karandinga kuingia rumande baada ya kukosa dhamana kutokana na wajeruhiwa wawili kati ya wale watatu kuwa katika hali mbaya hospitali ya mkoa wodi namba 5. |
 |
Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Manispaa ya Iringa wakitokea Mahakamani kuelekea Kituo cha Polisi Iringa wakienda kutaka kupata maelezo juu ya Mlalamikiwa Mh. Diwani Idd Chonanga ambaye ndiyo mlalamikiwa wa kwanza kutofikishwa Mahakamani baada ya kukamatwa na Polisi na kuachiwa kwa dhamana. Kaimu Kamanda wa Mkoa akiri kutofikishwa kwa Mh. Diwani Idd Chonanga mahakamani leo kwa kuwa aliachiwa kwa dhamana jana katika kituo cha Polisi na kuahidi Mh. Huyo atafikishwa mahakamani kesho tarehe 16/05/2012. Maelezo hayo alipewa Mheshimiwa Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa (Chadema) baada ya kuonana na Kaimu Kamanda ofisini kwake leo. |
Advertisement
hapa