Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » ALIYEKUWA NA MATUNDU MA3 KWENYE MOYO AFARIKI

ALIYEKUWA NA MATUNDU MA3 KWENYE MOYO AFARIKI

Written By mpekuaji on Friday, June 8, 2012 | 7:51:00 PM

Marehemu  Neema (kushoto) enzi za uhai wake alipotembelewa na  Albert G. Sengo aliyefika nyumbani kwa bibi wa mtoto huyu eneo la Butimba mkoani Mwanza kwa ajili ya kuchukuwa taarifa za kuomba msaada.
*****
Mtoto Neema George (16) amefariki dunia leo asubuhi majira ya saa moja huko wilayani Sengerema ambako ndiko wazazi wake wanaishi. 

Mtoto huyu aliyetajwa kuwa na matundu matatu kwenye moyo (kwa mujibu wa vipimo) hivi karibuni akiwa na wazazi wake walijitokeza katika blogu hii na kuomba wasamaria wema kujitokeza kumchangia fedha ili akapate matibabu ya moyo nchini India.

Taarifa za kiuchunguzi zinasema kuwa moyo wa marehemu Neema ulifikia hali ya kushindwa kutambua na kutofautisha kati ya damu safi na damu chafu na kama inavyojulikana kuwa kazi ya moyo ni kusukuma damu safi kwenda sehemu mbalimbali za mwili, pia damu chafu kuifanya ikasafishwe kwenye kibofu, ini na mapafu basi zoezi lote hili lilikuwa limefeli kwenye moyo wa mtoto huyo.

Marehemu Neema anatarajiwa kuzikwa kesho wilayani Sengerema.

Japo imeshindikana kunusuru maisha ya mwanae, baba wa marehemu aitwaye George Lenatus Mugunga amewashukuru wasamaria wema waliojitokeza kumsaidia.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts