STAA wa filamu Bongo, Tamrina Posh ‘Amanda’ hivi karibuni alizua songombingo la aina yake baada ya kukamatwa na Askari wa Usalama Barabarani ‘trafiki’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho hakikupenda jina lake liandikwe , tukio hilo lilitokea Mbezi Africana jijini Dar ambapo staa huyo alikuwa akiendesha gari lake dogo na ndipo aliposimamishwa na trafiki aliyemuomba amuoneshe leseni yake ya udereva.
“Kwa kuwa Amanda hakuwa na leseni halisi, yaani alikuwa na fotokopi ndipo mabishano yalipoanzia na kusababisha songombingo iliyochukua dakika kadhaa.
“Wakati wakiendelea kuzozana alifika trafiki mwingine ambaye alionekana kuwa juu ya yule wa kwaza akatatua tatizo hilo,” kilisema chanzo hicho.
Amanda alipotafutwa kwa njia ya simu, alikiri kutokea kwa kashikashi hiyo lakini akasema walimalizana palepale.
Post your Comment


