Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » KASHI ABANWA ARUDISHE MICHANGO YA NDOA YAKE BAADA YA MCHUMBA WAKE KUINGIA MTINI

KASHI ABANWA ARUDISHE MICHANGO YA NDOA YAKE BAADA YA MCHUMBA WAKE KUINGIA MTINI

Written By mpekuaji on Friday, June 8, 2012 | 12:07:00 PM

MSANII wa filamu Bongo, Jaji Hamisi ‘Kashi’ hivi karibuni amejikuta kwenye wakati mgumu kufuatia kubanwa na baadhi ya watu wake wa karibu arudishe michango ya harusi yake iliyoyeyuka baada ya mchumba wake kuingia mitini.

Rafiki wa karibu wa msanii huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake aliuambia mtandao huu kuwa, baadhi ya mashoga wa Kashi wamekuwa wakimpigia simu wakimwambia kama ndoa haipo awarudishie fedha zao.

“Kwa kweli sasa hivi Kashi yuko kwenye wakati mgumu sana, si unajua walimchangia ili kufanikisha harusi yake? Sasa baada ya ndoa yenyewe kuyeyuka, watu wanataka kurudishiwa fedha zao,” alidai mtoa habari huyo.

Baada ya mwandishi wetu kunyetishiwa juu ya habari hii, alimtafuta Kashi na alipopatikana alifunguka kuwa, ni kweli ameamua kuachana na mwanamume aliyetaka kumuoa kutokana na kubaini kuwa hakuwa na msimamo.

“Mimi niliamua kujinasua mapema kutokana na kuona kabisa mwanaume hana msimamo, kuhusu hilo la kubanwa nirudishe michango nitajua jinsi ya kuweka mambo sawa,” alisema Kashi.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts