Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » Mchumba wa Oprah Winfrey azikataa $100M ili kurusha harusi yao kwenye TV

Mchumba wa Oprah Winfrey azikataa $100M ili kurusha harusi yao kwenye TV

Written By mpekuaji on Thursday, June 7, 2012 | 7:05:00 PM

Mchumba wake na Oprah Winfrey Stedman Graham amedaiwa kukataa kuioenesha harusi yao kwenye TV.
Awali mwenzi huyo wa siku nyingi wa malkia wa Talk Show duniani, alidaiwa kukubali kupokea mamilioni ya dola kutoka Oprah, ili amruhusu kuirusha harusi yao kwenye kituo chake cha TV.

Sababu hasa ya kutaka kuonesha harusi hiyo ni kuvutiwa watazamaji kwenye kituo chake cha OWN ambacho kimeshuka umaarufu, lakini Stedman anadaiwa kubadilisha mawazo yake.


“Steadman alitaka kufanya lolote analoweza kusaidia kuongeza utazamwaji wa kituo hicho lakihi hakubaliani na wazo la kuweka maisha yao private mbele ya umma. Na pesa sio kitu ambacho kingemfanya akubali – Stedman ni millionare tayari,” chanzo kimoja kimeliambia the National Enquirer.

“Lakini ni mtu msiri sana, kufunga ndoa na Oprah ndio kitu pekee alichokuwa akikitaka kwa miaka mingi lakini wazo la kufanya ndoa yao ivutie utazamwaji wa TV ya Oprah lilimkata stimu.”

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts