Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » Beyonce, Jay & Blue wapanga kwenye nyumba ya dola 400,000 kwa mwezi!

Beyonce, Jay & Blue wapanga kwenye nyumba ya dola 400,000 kwa mwezi!

Written By mpekuaji on Tuesday, July 31, 2012 | 1:48:00 PM

Bedroom Eneo la ndani ya nyumba Jiko Masuala misosi hufanyika hapa Muonekano wa mbali wa nyumba hiyo ya kifahari Nyumba ina bwawa kubwa mbele yake
Sean Carter aka Jay-Z, mke wake mrembo Beyonce Knowles na mtoto wao Blue Ivy Carter wameamua kubadilisha mazingira kwa kupanga kwenye nyumba ya kifahari huko The Hamptons ambapo watakuwa wakilipa dola laki nne kwa mwezi.


Kiasi hicho ni zaidi ya shilingi milioni 630. It’s not a joke!
The Hamptons ni kundi la vijiji na makazi kwenye miji ya Southampton na East Hampton, ambayo huunda tawi la kusini la eneo la Long Island, New York. 


The Hamptons inajumuisha makazi aghali zaidi nchini Marekani.


Familia hiyo ya Jay-Z itakaa kwenye nyumba hiyo wote wa August.


Kwa mujibu wa gazeti la The New York Post, wapenzi hao na mtoto wao wa miezi saba wameikodi nyumba hiyo yenye 31,000-square-foot eneo la Bridgehampton ijulikanayo kama Sandcastle.


Nyumba hiyo ya kifahari ipo sokoni na inauzwa dola milioni 43 japo Bey na Jay wanataka kupumzika tu kwenye muda huu wa kiangazi.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts