Habari zenu, jamani mimi ni mara ya kwanza kuleta tatizo hapa, ni matumaini yangu nitafaidika na ushauri wenu. Mimi ni mwanaume nina miaka 26 , nafanya kazi kwenye kampuni moja hapa nchini.
Hivi karibuni hapa kazini kuna Mkuu wangu wa kazi ambaye ni mama mtu mzima amekuwa akinitaka kimapenzi.Yeye ni mke wa mtu na ana watoto.Mume wake hutumia muda mwingi katika shughuli za kibiashara nje ya nchi.
Hivi karibuni amekuwa karibu sana na mimi.Ukifika muda wa chakula huwaagiza wahudumu wa cafe waniletee chakula ofisini eti kwa sababu nipo busy na kazi.
Mara nyingi huja ofisini kupiga stori na mimi,jambo linalonofanya nikose amani mbele ya wenzangu.
Kuna siku moja alikuja nilipokuwa nimekaa ofisini kwangu akaniwekea mkono begani halafu akaniangalia usoni kwa sekunde kadhaa karibu nianguke kwa uoga.Japo hajanitamkia ila nahisi ananitaka kimapenzi maana ni wazi kabisa.
Jumatano ya wiki iliyopita alinisubiri mpaka nikamaliza kazi,then kanipa lifti mpaka maeneo fulani karibu na nyumbani kwangu.Wakati anaondoka akaniambia kuwa kuna safari ya kiofisi itabidi niende naye Mwanza wiki ijayo kwa ndege, kwa hiyo nijiandae.Yaani nime changanyikiwa sana.
Ijumaa aliniachia ujumbe ofisini eti tukutane lunch. kufika kaniodea na chakula nikabaki nimeduwaa.
Nilimuambia sitaweza kukaa kula maana nina kazi kibao ofisini nitabeba basi na yeye kabeba chake kaja kula ofisini kwangu alivyomaliza akakaa nikawa najaribu kupoteza lengo namuuliza mambo ya kazi lakini mara anishike mkono, mara aniangalie tu kwa muda usoni ili mradi tu ni kama mwanaume anavyomtongoza mwanamke vile.
Sasa najiuliza nimuelezaje huyu mama kuwa mimi sipo tayari na sitaki kwenda naye Mwanza . Mimi binafsi nina mchumba wangu ambaye tumetambulishana kwa wazazi.Niliona kuwa kabla hatujafunga ndoa ni bora nitafute kazi ili maisha yasitushinde.Bahati mbaya kazi inanitesa na kunipa mtihani mgumu
Nimechanganyikiwa na sijui cha kufanya.Nikifikiria nihame ofisi ,najiuliza ntapata wapi tena kazi na elimu yenyewe yakuunga unga.
Kilichonifanya nishtuke ni kadi aliyoninunulia siku chache zilizopita ,yaani ilikuwa ni ya kimapenzi kabisa . Wenzangu ofisini wameshaanza kuhisi vibaya.Nifanyaje jamani.Naomba ushauri wenu kupitia blog yenu
Post your Comment



